Mkurugenzi
wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo
jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi.
Ruth Minja.
Meneja wa
Takwimu za Bei na Ajira toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa
taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jjijjini Dar es Salaam,
kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MATUMIZI ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/2012 kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2007.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi
wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kutokana na hali hiyo kunaashiria
kupungua kwa umasikini wa kipato kwenye kaya kwa kuelekeza matumizi
mengine bidhaa zisizo za vyakula kama usafiri, mawasiliano, makazi, maji
pamoja na nishati.
Amesema matokeo yanaonyesha kwamba mizania ya matumizi ya kaya
kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/2012
kutoka asilimia 47.8 mwaka 2007.
Amesema kumekuwa na ongezeko la zaidi ya mara mbili ya matumizi ya
kaya kwenye kundi la Mawasiliano asilimia 5.6 ikilinganishwa na
asilimia 2.1 ya mwaka 2007.
Nae Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Ruth Minja amesema baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika kupata
Fahirisi za bei zinzoonyesha uhalisia wa matumizi ya kaya binafsi kuwa
ni pamoja na mizania katika bidhaa za huduma muhimu ikiwemo Vyakula,
afya, Usafiri, Maji na Nishati.
No comments:
Post a Comment