Mtafiti
Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania kutoka Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk. Emmarold Mneney (kushoto),
akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Salama kilichopo Kata ya Ng’haya
baada ya kupokea changamoto zao katika mkutano uliofanyika kijijini hapo
juzi.
Mtafiti
Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk.
Nicholaus Nyange (kulia), akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Salama
kilichopo Kata ya Ng’haya kuhusu matumizi ya Bioteknolojia.
Mratibu
Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Utunge kutoka nchini
Kenya (kulia), akiwa katika mafunzo hayo ya matumizi ya Bioteknolojia
katika kilimo yaliyofanyika kijiji cha Salama wilayani Magu. Kushoto ni
Mwanahabari wa gazeti la majira jijini Mwanza.
Mtafiti
Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania kutoka Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk. Emmarold Mneney (kulia), akisisitiza
jambo wakati akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Bugatu wilayani Magu
mkoani Mwanza baada ya kupokea changamoto zao za kilimo.
Wakulima
wa Kijiji cha Bugatu wilayani Magu mkoani Mwanza wakiwa kwenye mafunzo
hayo baada ya kueleza changamoto zao za kilimo kwa watafiti kutoka
Costech na Jukwaa la Bioteknolojia.
Mtafiti
Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk.
Nicholaus Nyange (kulia), akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Ng’haya
kilichopo Kata ya Ng’haya kuhusu matumizi ya Bioteknolojia.
……………………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale, Magu
WAKULIMA
wa Kijiji cha Salama kilichopo Kata ya Ng’haya wilayani Magu mkoani
Mwanza wamewatupia lawama maofisa ugani wakidai wamekuwa wakichangia
kuporomosha kilimo kwa kuwa hawafiki kuwapa elimu ya kilimo.
Malalamiko
hayo waliyatoa mbele ya Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (Costech) na waandishi wa habari katika ziara ya watafiti hao
mkoani humo ya kujua changamoto zinazo wakabili na kuzitafutia
ufumbuzi.
Watafiti
hao wako katika ziara hiyo mkoa wa Mwanza na Mara ya kukukutana na
wakulima na kutoa mafunzo ya matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo kwa
kuwezeshwa na Jukwaa la Bioteknolojia ambapo walifanikiwa kukutana na
wakulima wa Kijiji cha Salama, Bugatu na Ng’haya vyote vikiwa wilayani
Magu huku changamoto zao zikilingana.
Mmoja
wa wakulima wa kijiji hicho Kaabi Mahushi alisema changamoto kubwa
waliyonayo katika kilimo ni elimu ya kilimo kwani maofisa ugani
hawawafikii hivyo kujikuta wakikosa ushauri kuhusu masuala ya kilimo cha
mazao yote.
“Changamoto
kubwa tuliyonayo ni kutofikiwa na maofisa ugani tunaiomba serikali
kutuletea maofisa hao ili tuweze kupata ushauri wao” alisema Mahushi.
Mkulima
Musa Mnyalo alisema ukosefu wa pembejeo, mbegu bora na wataalamu hilo
ni eneo jingine linalo warudisha nyuma katika kilimo cha mpunga, pamba,
mahindi, mihogo na choroko ambayo yamekuwa yakishambuliwa na magonjwa
ikiwemo batobato kwa zao la mihogo.
William
Pastory alisema bei ya mbegu ya pamba kwa kilo 6 kuuziwa sh.20,000 ni
ghari mno ukilinganisha kuwa bei ya zao hilo imekuwa ikishuka kila
wakati kutoka sh.1200 hadi kufikia 700 kwa kilo.
Changamoto
zingine zilizotajwa na wakulima hao ni pamoja na kukosekana kwa mbegu
bora ya pamba, mazao yao kama mahindi, mihogo, mpunga kushindwa kustawi
kutokana na kushambuliwa na wadudu, ukame, ukosefu wa mvua na madawa.
Akizungumza
baada ya kupokea changamoto hizo kutoka kwa wakulima hao Mtafiti Mkuu
wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (Costech) Dk. Emmarold Mneney alisema Serikali inajua hicho
kiliochao na ndio maana imetenga fedha zinazo wasaidia watafiti kufanya
utafiti wao utakaotoa majibu ya kuwakomboa wakulima.
“Hivi
sasa tupo katika tafiti za mbegu ya mahindi na pamba wakati wowote
tutapata majibu yatakayosaidia kupata mbegu bora kwani tafiti
zinafanyika katika maabara ya ndani na zikitoa matokeo mazuri
tutazalisha mbegu hizo kwa wingi na kuwasambazia wakulima” alisema
Dk.Mneney.
Mtafiti
Kiongozi wa Costech Dk.Nicholaus Nyange alisema licha ya Tanzania kuwa
na changamoto ya mbegu za pamba nchi kadhaa kama, Afrika Kusini, India,
Bakinafaso na Sudani zimefanikiwa katika kilimo hicho baada ya kutumia
Bioteknolojia ya uzalisha ambayo anashauri serikali, Bodi ya Pamba na
wadau wengine kuhawilisha teknolojia hii iweze kutumika hapa nchini
No comments:
Post a Comment