Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango (katikati) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein
Katanga (kushoto) mfano wa hundi wakati wa makabidhiano ya fedha hizo
mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba
na Sheria Amon Mpanju (kulia) mfano wa hundi wakati wa makabidhiano ya
fedha hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Katanga.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa
makabidhiano ya fedha zilizotolewa kwa Mahakama leo jijini Dar es
salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon
Mpanju na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (kushoto).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Katiba na Sheria Amon Mpanju (kulia) akitoa shukrani baada ya kupokea
mfano wa hundi aliyopokea kwa lengo la kusaidia mahakama leo jijini Dar
es salaam. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein
Katanga akitoa shukrani baada ya kupokea mfano wa hundi aliyopokea kwa
lengo la kusaidia mahakama leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na kulia ni
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakiendelea na kazi yao wakati wa makabidhiano ya fedha hizo mbele ya
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO
………………………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
Dar es salaam.
Serikali imeikabidhi Mahakama ya
Tanzania kiasi cha Sh.bilioni 12.3 zilizoahidiwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho
ya Siku ya Sheria kwa lengo la kuiwezesha Mahakama kuimarisha utendaji
kazi na kutekeleza majukumu yake inapasavyo.
Akikabidhi fedha hizo mbele ya
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Philip Mpango amesema kuwa fedha zilizokabidhiwa kwa Mahakama ni
mwitikio wa kutekeleza ahadi ya Rais aliyoitoa wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Sheria Duniani Januari 4, 2016.
“Ni matumaini ya Serikali fedha hizo zitatumika vizuri na zitatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa” alisema Dkt. Mpango.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju amemshukuru Mhe. Rais kwa kwa
kutekeleza ahadi aliyoitoa ndani ya siku nne na kuudhihirishia umma kuwa
kauli mbiu ya “Hapa Kazi Tu” anaisimamia kwa vitendo.
Naye Mtendaji Mkuu wa Mhakama
Hussein Katanga amesema kuwa fedha walizokabidhiwa zitasaidia ujenzi wa
mahakama nchini na zipo ndani ya bajeti ya mwaka 2015/2016 na
watazitumia kulingana na malengo yaliyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment