Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, February 16, 2016

JESHI LA POLISI LA WASHIKILIA WAHARIFU SUGU NA WANAOUZA CD ZA NGONO ZA UTUPU NJOMBE

 KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE WILBROAD MUTAFUNGWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Linawashikilia  Watu   Watatu Wanaodaiwa Kuwa Ni Majambazi  Sugu  Wa Uvunjaji   Mjini Njombe  Baada Ya  Jeshi Hilo Kuendesha Msako  Na  Doria  Uliofanyika Kuanzia Majira Ya Saa Nne Hadi Saa Sita  Ya Usiku  Ambao Ulifanyika  Februari 15  Na Kuwakamata Watuhumiwa  Hao.

Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Amewataja  Watuhumiwa Hao Kuwa Ni Pamoja Na  Yusuph Yohana Mwenye Umri Wa Miaka 32 Mkazi Wa Mtaa Wa Matalawe Pamoja Na Salumu Idd   Mwenye Umri Wa Miaka 21     Na Saibu Salumu  Mwenye Mwenye Umri Wa Miaka 28 Wote Wawili Wakazi Wa Dar Es Salaamu Ambao Kwa Njombe Wanaishi Mtaa Wa National Housing.

Aidha Kamanda Mutafungwa Amesema  Watuhumiwa Hao Walikamatwa Katika Mtaa Wa  Matalawe  Mjini Njombe  Wakiwa Na Kete Tatu Za Bangi Pamoja Na Mali Ya  Kanisa Katholiki  Nazarethi  Senta Jimbo La Njombe  Ambapo Miongoni Mwa Mali Walizokutwa Nazo Ni  Flati Screen,Monita,King'amuzi Cha Azam,Printer,Radio Na Deck Aina Ya Singsung.

Katika Hatua Nyingine Kamanda Mutafungwa Amesema Jeshi Hilo  Linamshikilia  Mkazi Wa Mtaa Wa Kwivaha Leonard Kyomo  Aliyekamatwa Katika Msako Huo  Baada Ya Kukutwa  Anauza  CD 102 Za Picha Za Ngono    Kwenye Duka Lake  Nakwamba Uchunguzi Ukikamilika  Watuhumiwa  Wote  Watafikishwa Mahakamani Kujibu Tuhuma Zinazowakabili.

Mbali Na Tukio Hilo Kamanda Mutafungwa Amesema  Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Linaendelea Kuchunguza Kifo Cha  Mashaka Cha Mkazi Wa Kijiji Cha Lupanga Tarafa Ya Mawengi Anamaria Mganwa  Mwenye Umri Wa Miaka 45  Ambaye Amekutwa Akiwa Amefariki  Kichakani  Huku Mwili Wake Ukiwa Hauna Majeraha Yoyote.

Amesema Marehemu Anamaria Mganwa Aliondoka Nyumbani Kwake Mnamo Februari  12  Mwaka Huu  Na Alipoondoka  Alimuaga Mme Wake  Kwamba Anakwenda Kutafuta Vibarua Vya Kulima   Na Hakurudi Hadi Alipokutwa Akiwa Amefariki  Ambapo Jeshi Hilo Linaendelea Kuchunguza Chanzo Cha Kifo Hicho.

No comments:

Post a Comment