Na Mwandishi wetu, Iringa
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Iringa zimesomba mashamba na nyumba na kuwaacha wananchi wengi wakiwa hawana mahali pa kukaa.
Vitongoji vilivyo athirika sana ni Kisanga, Nyallu, Makoka na Mbughani. Mpaka sasa bado idadi isiyo rasmi inakadiliwa watu zaidi ya 200 bado wamezingirwa na maji siku ya 4.
Juhudi za uokoaji zikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela zimefanikiwa kuokoa watu 399 kitongoji cha Kisinga, watu 38 kutoka kitongoji cha Makoka, na watu 23 kutoka kitongoji cha Nyalu. Jeshi la polisi lilitoa helicopter kusaidia uokoaji na pia kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilikuwa mstari wa mbele kwenye zoezi hilo.
Maeneo mengi yalihitaji waogoleaji mahiri ili kuwafikia wananchi.
Zoezi linaendelea hado sasa. shule 2 zimetengwa kwa ajili ya kupokea wahanga wa mafuriko shule ya msingi Itunundu na shule ya msingi Kisanga.
kitongoji cha Nyalu wamezingirwa na maji
Nyumba za Kaya zaidi ya 80 za kitongoji cha kitanewa, kijiji cha mapogoro Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa zatakiwa kuhama
Nyumba
za Kaya zaidi ya 80 za kitongoji cha kitanewa, kijiji cha Mapogoro
Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa zipo hatarini kuathiriwa na mafuriko
endapo hazitahama eneo hilo ambalo ndipo mkondo wa maji ya Mto mapogoro
umechekupuka.
Kufuatia
hali hiyo serikali Wilayani Iringa imewataka wananchi hao kuhama eneo
hilo na kuhamia kwenye eneo lililotengwa kijiji cha Mapogoro hadi mvua
zitakaposimama na kujenga makazi ya kudumu huko kijijini.
Taarifa
zaidi na Irene Mwakalinga kutoka Iringa
Hapa ni kazi ya kurejesha mkondo wa maji kwenye njia yake ya asili
ikiendelea kwa kuchimba mchanga na kupanua kingo ya bonde ambalo mto
umehamia na kuziba maji yasiendelea kwenda kwenye makazi ya watu.
Aidha
Kinachoonekana hapa ni moja ya shamba la mahindi na karanga ambalo
limegeuka mto na kumegwa ardhi yake na kasi ya maji ambayo inaendelea
kula ardhi hiyo.
Afisa
Tarafa wa Idodi Yakub Kiwanga amesema kuwa mkondo wa maji ya Mto huo
umehama kutoka eneo la mtitiririko wake awali na kukatisha kwenye maeneo
ya makazi ya watu ikiwa ni miaka zaidi ya 40 tangu mto huo ulipohama
tena.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongwea na na waathirika wakati wa zoezi la uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga
Kijiji cha Itunundu ndio kambi kubwa ya uokoaji
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongwea na na waathirika
wakati wa zoezi la uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji
cha Pawaga
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongwea na na waathirika wakati wa zoezi la uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akikagua athari katika kijiji cha Mapogoro Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akiendelea kukagua athari
katika kijiji cha Mapogoro Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa
No comments:
Post a Comment