KATIBU CCM WILAYA SADAKATT KIMATI AMESEMA ANAYO HAKI YA KUJIVUNIA KWANI CHAMA CHA CCM MKOA WA NJOMBE HUSUSANI WILAYA YAKE MIJI MIWILI NA MAJIMBO YA VIJIJINI YANAONGOZWA NA WENYEVITI WA CCM NA CHAMA HICHO KINA NGUVU KUBWA NA HAKIWEZI KUTETELEKA.
KATIBU WA CCM WILAYA YA NJOMBE BWANA SADAKATT KIMATI AKIZUNGUMZA NA MTANDAO HUU AKIWA KATIKA OFISI YAKE AMBAPO AMESEMA WAKATI WA KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA KUTIMIZA MIAKA 39 YA KUZALIWA KWA CHAMA HICHO KUNA ZAIDI YA WANACHAMA ELFU KUMI WAMEJIUNGA NA CHAMA HICHO KATIKA MAENEO MBALIMBALI NA KUFANYA ZAIDI YA WANACHAMA ELFU 80 WA CCM WAPYA NA WA ZAMANI.
Zaidi Ya Wanachama Elfu Kumi Wa CCM Wilayani Njombe Wamefakiwa Kurudisha Kadi Za Vyama Vyao Na Kujiunga Na Chama Hicho Katika Kipindi Cha Siku Sita Wakati Wa Kuelekea Kilele Cha Maadhimisho Ya Kutimiza Miaka 39 Ya Kuanzishwa Kwake Ambapo Shughuli Mbalimbali Zilifanyika Na Wanachama Hicho.
Akizungumza Na Uplands Fm Katibu Wa CCM Wilaya Ya Njombe Sadakat Kimati Amesema Uzinduzi Wa Kuelekea Kilele Cha Maadhimisho Ya Kutimiza Miaka 39 Ulifanyika Januari 31 Na Kilele Chake Kinatarajiwa Kuwa Kesho Februari 6 Kitakachofanyikia Katika Kijiji Cha Itulike Tawi La Ipuyi Kata Ya Ramadhani Mjini Njombe.
Aidha Katibu Huyo Sadakat Kimati Amesema Katika Kuelekea Kilele Hicho Chama Cha Mapinduzi Kimefanikiwa Kutekeleza Majukumu Mbalimbali Ikiwemo Kutembelea Hospitali Ya Kibena Na Vituo Vya Afya Kwaajili Ya Kuwajulia Hali Wagonjwa Na Kukabidhi Misaada , Kufanya Usafi Wa Mazingira Na Kupanda Miti Ya Mbao Na Matunda .
Amesema Chama Cha Mapinduzi Kilipatikana Baada Ya Kuungana Kwa Vyama Viwili Chama Cha ASP Yaani Afro Shiraz Part Na Chama Cha TANU Yaani Tanganyika African National Union Tangu Mwaka 1977 Ambapo Wakati Huo Kilikuwa Kichanga Lakini Kwa Sasa Hakipaswi Kuitwa Kichanga Bali Ni Chama Kongwe Nchini Tanzania.
Kwa Upande Wake Katibu Mwenezi CCM Wilaya Ya Njombe Hiltra Msola Ametoa Ratiba Itakavyokuwa Kwenye Maadhimisho Ya Kutimiza Miaka 39 Ya Kuzaliwa Kwa Chama Cha Mapinduzi Kwamba Watakao Husika Ni Viongozi Wote Wa Chama Na Serikali Mkoa ,Madiwani Na Wanachama Wa Kawaida.
Bwana Msola Amesema Wanachama Na Wananchi Wataingia Kwa Maandamano Makubwa Kutoka Barabara Kuu Ya Kuelekea Wanging'ombe Hadi Kwenye Eneo La Tawi La CCM La Ipuyi Itulike.
Kilele Cha Maadhimisho Ya Kutimiza Miaka 39 Ya Kuzaliwa Kwa Chama Hicho Kinatarajia Kufanyika Kesho Ambapo Kimkoa Na Wilaya Ya Njombe Kitafanyikia Katika Kata Ya Ramadhani Kijiji Cha Itulike Tawi La Ipuyi.
No comments:
Post a Comment