Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL) Mwanza, Raymond Richmond,akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu kampuni hiyo kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya
pamba,kama chanzo cha nishati ya umeme kinachotumika kuendeshea
mitambo.Kushoto ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday
Kidolezi.
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya
Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond, akizungumzia mradi wa matumizi ya
mapumba ya mchele na mashudu ya pamba,ambacho ni chanzo cha nishati ya
kuendesha mitambo kiwandani hapo.Nishati ni rafiki wa mazingira kwa
sababu haina hewa ukaa.Wanaokoa Dola za Kimarekani (USD) 400,000 hadi
500,000 kwa mwaka ambazo zingetumika kununua mafuta mazito na dizeli ya
kuendeshea mitambo .
Waandishi wa habari wakiongozwa na
Meneja wa Kiwanda cha kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond(wa
kwanza kushoto), kwenda kutembelea mtambo unaotumia mapumba ya mchele
na mashudu ya pamba kuzalisha nishati ya umeme inyotumika kuendesha
mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa TBL,
Sunday Kidolezi.
Meneja wa Nishati na Maji wa
Kampuni ya Bia (TBL)Mwanza, Sunday Kidolezi (wa kwanza kulia),wakiwa na
waandishi wa habari wakati wakitembelea mtambo wa kuzalisha umeme kwa
kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.wa Kwanza kutoka kushoto
(mwenye shati jeupe), Ni Meneja wa Kiwanda hicho, Raymond Richmond.
Meneja wa Kampuni ya Bia (TBL)
Mwanza,Raymond Richmond (mwenye shati jeupe) akiwaonesha waandishi wa
habari mtambo unaozalisha nishati ya umeme kwa kutumia mapumba ya mchele
na mashudu ya pamba kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kiwanda
hicho.anaoshuhudia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo,Sunday
Kidolezi (mwenye fulana ya mistari).Mwingine ni mwandishi wa habari wa
kampuni ya The Guardian, Daniel Mkate,ambaye ni miongoni mwa waandishi
wa habari waliotembelea kiwanda hicho.
Raymond Richmond, Meneja wa
kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo
pichani), mapumba ya mchele,yanayotumika kuzalisha nishati ya umeme wa
kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa
kampuni hiyo.
Mwandishi wa habari, Daniel Mkate
(kushoto) akiwauliza maswali, Meneja wa Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,
Raymond Richmond na Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday
Kidolezi, kuhusu changamoto ya upatikanaji wa mali ghafi hiyo na
madhara yake katika kuzalisha nishati na athari za mazingira.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni
ya Bi (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba kwenye magunia, kabla ya kuingizwa
kwenye mtambo wa kuzalisha umeme kiwandani hapo.Hapo ni katika eneo
linalotumika kupakulia shehena ya mapumba hayo ya mchele, kutoka kwa
msambazaji.
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya
Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmod, akiwaonyesha waandishi wa habari,
Daniel Mkate wa TRhe Guardian (nyuma) na Henry Kavirondo wa Chanel
Ten,mashine inayosukuma mapumba ya mchele na mashudu ya pamba, kwenda
kwenye mtambo wa kufua umeme unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda
hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday
Kidolezi.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni
ya Bia (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba ya mchele kwenye mashine kwa ajili
ya kuyasukuma kadi kwenye mtambo wa kuzalisha nishati ya umeme,
unaotumiwa kuendesha mitambo ya uzalishaji ya kiwanda hicho.
Meneja wa Maji na Nishati wa
kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Sunday Kidolezi, akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari kuhudu mradi huo wa uzalishaji wa nishati
ya umeme,unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda cha kampuni hiyo kwa
kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.Wa kwanza kushoto ni
Meneja wa kiwanda cha kampuni hiyo,Raymond Richmond.
No comments:
Post a Comment