Majeruhi 15 Wamelazwa Katika Hospitali Ya Kibena Kutokana Na Ajali Iliyotokea Jana
Majira Ya Saa Moja Usiku Eneo La Mto Yakobi Ikilikutanisha Basi La Kampuni Ya New
Force Lenye Namba Za Usajili T 418 DDT Inayofanya Safari Zake Za Dar Es Salaama
Songea Kufuati Dereva Wa Basi Hilo Kuwa Na Mwendo Kasi.
Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Amethibitisha
Kutokea Kwa Tukio Hilo Na Kusema Kuwa Chanzo Cha Ajali Hiyo Ni Mwendo Kasi Wa
Dereva Wa Basi La New Force Na Loli Ambalo Lilikuwa Mbele Yake Lililokuwa
Limekwama Breki Na Kushindwa Kuweka Alama Barabarani.
Aidha Kamanda Mtafungwa Amesema Kuwa Basi Hilo La New Force Lililokuwa
Likiendeshwa Na Godfrey Mahenge Ambaye Naye Ni Miongoni Mwa Majeruhi 15 Liliacha
Njia Na Kutumbukia Mtoni Na Kusababisha Majeruhi Hao Baada Ya Kushindwa Kufunga
Breki Ghafra Alipoona Mbele Yake Kuna Loli Lenye Namba T 573 CDD.
Kamanda Mutafungwa Amesema Dereva Wa Basi La New Force Anahojiwa Licha Yakuwa
Anaendelea Kupata Matibabu Huku Dereva Wa Loli Namba T 573 CDD Aina Ya Enveko
Mali Ya Kampuni Ya Otawa Akitafutwa Baada Ya Kukimbilia Kusikojulikana Ambapo Jeshi
La polisi Likiwataka Wamiliki Na Madereva Kuzingatia Sheria Za Usalama Barabarani.
CUE....KAMANDA AJALI
Kwa Upande Wake Majeruhi Wakizungumza Wakiwa Katika Hospitali Ya Kibena Mapema
Leo Wamesema Kuwa Basi Hilo La New Force Lilikuwa Mwendo Kasi Na Kufanya Dereva
Kushindwa Kuhimili Kusimama Ghafra Mara Lilipoonekana Loli Limesimama Mbele
Yake Likiwa Limekatika Breki Na Kusababisha Kupinduka Kwa Basi Hilo.
CUE.....MAJERUHI
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Kupitia Kitengo Cha Usalama Barabarani Limekuwa
Likitoa Elimu Ya Usalama Barabarani Kwa Madereva Na Wamiliki Wa Vyombo Vya Moto
Kupitia Kituo Cha Radio Uplands Fm Kila Siku Ya Juma Tano Asubuhi Lakini Bado
Inaonekana Sheria Hizo Kupuuzwa Na Madereva.
Tukio Hilo La Ajali Limetokea Ikiwa Ni Siku Chache Tu Zimepita Tangu Jeshi La Polisi
Kupitia Kitengo Cha Usalama Barabarani Kuadhimishi Kilele Chake Ambacho Mgeni
Rasmi Alikuwa Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dtk Rehema Nchimbi Ambaye Alitaka Sheria
Za Barabarani Kufuatwa Na Madereva .
No comments:
Post a Comment