Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) imepokea vifaa mbalimbali vikiwemo vibanda vya kupigia kura
(vituturi), masanduku ya kupigia kura, lakiri za kufungia masanduku pamoja na vifaaa
vingine vitakavyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu nchini.
Hayo yamesemwa na Kaimu
Mkurugenzi Ununuzina Ugavi Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Eliud Njaila alipokuwa
akiongea na waadishi wa habari wakati wa kupokea vifaa hivyo leo jijini Dar es
salaam.
“Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda
kuwajulisha Watanzania na wadau wote wa uchaguzi kuwa maandalizi ya uchaguzi
mkuu wa mwaka huu yamekamilika na vifaa vyote muhimu vya kuendeshea zoezi hilo
vimekamilika” alisema Bw. Njaila.
Akisisitiza juu ya
gharama ya vifaa hivyo, Bw. Njaila alisema kuwa vifaa mbalimbali vya uchaguzi
zikiwemo karatasi za kupigia kura vyote kwa ujumla vinathamani ya Sh.
41,868,045,168 bila kuweka gharama ya
ununuzi wa mashine za BVR.
Aidha, Bw. Njaila
alisema kuwa vituturi vinaendelea kutengenezwa hapa nchini ambapo kila siku
idadi ya vituturi 8000 vitakuwa vinakabidhiwa kwa kwa tume ya uchaguzi tayari
kwa kusambazwa nchi nzima katika kila halmashauri kabla ya zoezi la kupiga kura
Oktoba 25 mwaka huu.
Vifaa kwa ajili ya
zoezi la uchaguzi vitasambazwa kwa kanda kuanzaia kanda ya Ziwa, kanda ya kati,
kanda ya kusini, kanda ya magharibi, kanda ya nyanda za juu kusini, kanda ya
kaskazini, kanda ya mashariki pamoja na Zanzibar kulingana na utaratibu
uliowekwa na NEC na ZEC.
No comments:
Post a Comment