Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, September 9, 2015

MAAMUZI YA RUFAA ZA WABUNGE NA MADIWANI YALIYOFANYIKA KATIKA KIKAO CHA TUME

RUFAANI ZA WABUNGE NA MADIWANI,8-9-2015.pdf_page_1Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesikiliza na kuamua rufaa rufaa 6 za wabunge kati ya rufaa 13 zilizokuwa hazijafanyiwa maamuzi kutokana na vielelezo vyake kutokamilika. Kati ya rufaa hizo, Tume imezikataa sababu za rufaa zote na kukubaliana na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi. Hii ina maana kuwa maamuzi yaliyofikiwa na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo husika ndio utakaofuatwa. (Jedwali 1).
Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesikiliza rufaa za Madiwani 70 kati ya rufaa 118 zilizokuwa hazijafanyiwa maamuzi kutokana na vielelezo vyake kutokamilika. Kati ya rufaa 70 zilizoamuliwa jumla ya rufaa 14 zimekubaliwa na Tume na wagombea
waliokuwa wameenguliwa wamerudishwa kugombea. Hii ina maana kuwa Tume imetengua uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi na kuwarejesha wagombea katika kinyang’anyiro cha Udiwani katika Kata zao. Kwa rufaa 58 Tume imekataa sababu zilizotolewa na kukubali uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi. Hii ina maana kuwa wagombea watafuata maamuzi yaliyofikiwa na Wasimamizi wa Majimbo na Kata husika. (Jedwali 2)
Jedwali Na. 1: MAAMUZI YA RUFAA ZA WABUNGE
NA. JINA LA JIMBO JINA LA MRUFANI JINA LA MRUFANIWA UAMUZI WA TUME
1. TANDAHIMBA Likumbo Shaibu Salimu Katani Ahmad Katani Tume imekataa rufaa na
(CCM) (CUF) Wagombea wote waendelee na
Kampeni za Uchaguzi.
2. MWANGA Kilewo Henry John Prof. Maghembe Jumanne Tume imekataa rufaa na
(CHADEMA) Abdallah Wagombea wote waendelee na
Kampeni za Uchaguzi.
(CCM)
3. MWANGA Kilewo Henry John Msuya Youngsaviour Tume imekataa rufaa na
Anderson Wagombea wote waendelee na
NA. JINA LA JIMBO JINA LA MRUFANI JINA LA MRUFANIWA UAMUZI WA TUME
(CHADEMA) (NCCR – MAGEUZI) Kampeni za Uchaguzi.
4. WANGING’OMBE Lwenge Gerson Hosea Dismas Andrea Luhwago Tume imekataa rufaa na
(CCM) (CHADEMA) Wagombea wote waendelee na
Kampeni za Uchaguzi.
5. MJI HANDENI Daudi Killo Lisewa KigodaAbdallah Omari Tume imekataa rufaa na
(CHADEMA) (CCM) Wagombea wote waendelee na
Kampeni za Uchaguzi.
6. KASULU MJINI Bunyago Gideon NSANZUGWANKO DANIEL Tume imekataa rufaa na
Boniface (NCCR- NIKODEMUS (CCM) Wagombea wote waendelee na
MAGEUZI) Kampeni za Uchaguzi.

No comments:

Post a Comment