Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi wa mji wa Meatu mkoani Simiyu wakati alipofanya
mikutano mbalimbali katika wilaya za Busega, Meatu, Bariadi na Itilima
akiwaomba wananchi wa wilaya hizo kumpigia kura za ndiyo ili kuwa rais
wa Tanzania na kuwatumikia watanzania katika nafasi hiyo kubwa.
Amewaambia wananchi hao kwamba
ametekeleza miradi mbalimbali ya barabara nchini kwa mafanikio akiwa
Waziri wa Ujenzi na alikuwa akitumwa, Lakini sasa atakuwa akiwatuma
yeye watendaji na kuwasimamia. Jukumu ambalo yeye binafsi anaweza
kulitekeleza kwa mafanikio makubwa, uaminifu, uchapakazi na ukweli ili
kuleta maendeleo na mabadiliko ya kweli kwa watanzania wa kipato cha
chini lakini pia kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Ameongeza kwamba anataka Tanzania
iwe nchi ya viwanda ili kukuza ajira kwa vijana waliowengi na kukuza
uchumi wa taifa kuptia sekta hiyo ya viwanda ambapo ameelezea kwamba
serikali yake itajenga viwanda Vodogo, Vya kati na Vikubwa ambayo
vinaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali kama mikoba, mikanda, viatu, Nguo
na bidhaa nyingine nyingi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SIMIYU)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano wake wa kampeni mjini Meatu
mkoani Simiyu leo.
Umati wa wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo uliofanyika mjini Meatu mkoani Simiyu.
Baadhi ya Vijana wa Meatu wakiwa juu ya mti na bendera zao wakipata ujumbe wa Dr John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Akina mama wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Dr, John Pombe Magufuli.
Wananchi wakimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akimwaga sera zake.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiwasili kwenye uwanja wa mkutano mjini Meatu.
Msanii Emmanuel Mbasha akiwa katika mkutano huo.
Wasanii wa ngoma za kisukuma wakiwa wamevakia mithiri ya ndege aina ya Tai wakiwa katika mkutano huo ili kutoa burudani.
Kijana huyu akiwa amevaa kofia yake aina ya Pama huku ikiwa imevalishwa vipeperushi vinavyosema Magufuli “Hapa ni Kazi Tu”
Mgombea ubunge wa jimbo la Itilima Ndugu Silanga Njalu akiwaomba kura wananchi wa Nanga wilayani Itilima.
Mama huyu akionyesha mapenzi yake kwa mgombeaubunge wa jimbo la Itilima Ndugu Njalu Silanga.
Ngoma zimepigwa sasa ni wakati wa kusikiliza sera za Dr. John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Busega Paul Mzindakaya huku
Dr. Titus Kamani Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu akisikiliza wakati wa
mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Lamadi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi wa Lamadi mkoani Simiyu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM mkoawa Simiyu Dr. Titus Kamani wakati
alipokuwa akimnadi katika kijiji cha Mkula.
Hapa ni Magufuli tuuu!!
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiwasili katika mji wa Bariadi kwa ajili ya mkutano wa kampeni.
Mgombea ubunge wa jimbo la Busega Dk Chegeni akiomba kura mjini Lamadi Busega.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiwapigia debe wagombea ubunge na udiwani Meatu.
Msanii Mr Blue akitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Meatu leo.
Vijana wa Orijino Komedi wakitumbuza katika mkutano huo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akifurahia onesha la vijana wa orijino Komedi.
Shishi Baby Shilole akifanya vitu vyake jukwaani mjini Meatu wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika mjini humo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiondoka katika eneo la mkutano mara baada ya kumaliza kuhutubia
mkutano huo uliofanyika mjini Meatu mkoani Simiyu leo.
No comments:
Post a Comment