Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, August 23, 2015

JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LA HIMIZA MAZOEZI KWA WANANCHI KUIMARISHA MIILI YAO



 BAADA YA MAZOEZI TIMU NZIMA YA POLISI INARUDI KWENYE UWANJA WA GWARIDE






 KAMANDA WA POLISI MKOA WA NJOMBE WILBROAD MTAFUNGWA









 PUSHAPU KWA WOTE KUNYOSHA VIUNGO


 ASKALI POLISI WAKIWA NA ASKALI  MGAMBO WAKIWA KWENYE MAZOEZI HAPA NI BAADA YA KUKIMBIA MCHAKAMCHAKA








Wananchi Na Watumishi Wa Umma Wametakiwa Kutambua Umuhimu Wa Kufanya Mazoezi Kwaajili Ya Kujenga Afya Zao Ili Kupunguza Baadhi Ya Magonjwa Yanayosababishwa Na Kutofanya Mazoezi Ambapo Askali Wa Polisi Na Mgambo Kila Siku Za Juma Mosi Wanakuwa Mazoezini.

Akizungumza Na Askali Polisi Na Mgambo Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Njombe Wilbroad Mtafungwa Amesema Jamii Inatakiwa Kupunguza Uchomvu Na Magonjwa Yasiyo Ya Lazima Huku Wananchi Wakitakiwa Kuonesha Ushirikiano Kwa Polisi Katika Kufanya Mazoezi Na Kutokomeza Maovu.

Aidha Kamanda Mtafungwa Amepongeza Askali Na Baadhi Ya Askali Mgambo Ambao Wameitikia Mpango Wa Jeshi La Polisi Wa Kufanya Mazoezi Kila Siku Ya Jumamosi Ambapo Hata Jamii  Mjini Njombe Inaalikwa Kuungana Na Jeshi Hilo Kufanya Mazoezi Asubuhi.

Kamanda Mtafungwa Amesema Kuwa Jumamosi Ijayo Watashirikisha Maafisa Uhamiaji Na Waandishi Wa Habari Kufanya  Mazoezi Hayo Ambayo Yanaanza Kufanyika Saa Kumi Na Moja Alfajiri Na Kukamilika Saa Moja Asubuhi.

Mkuu Wa Kituo Cha Mazoezi Ya Mgambo Njombe Mjini Sajent Elias Banaba Matwani Amesema Kuwa Mazoezi Kwa Jeshi La Polisi Na Wananchi Ni Muhimu Huku Akisema Kuwa Raia Wanawatenganisha Askali Wa Polisi Na Askali Wa Mgambo Na Kutaka Kudumisha Umoja Wa Jeshi Hilo.

No comments:

Post a Comment