FRANK MUHANDO NI MENEJA WA MRADI IBB NYANDA ZA JUU KUSINI
MKURUGENZI MTENDAJI WA ACTN AFRIKA MHANDIS SAID MKOMWA
HAWA NI WASHIRIKI WASHIRIKI WA MAFUNZO YA KILIMO HIFADHI YALIYOTOLEWA NA SHIRIKA LA AGRA.
MKUFUNZI WA MAFUNZO KWA WAKULIMA KANDA YA KUSINI DEOGRATIAS NGOTIO AKIWAELIMISHA WAKULIMA HAO
WASHIRIKI WA MAFUNZO YA SIKU NNE WAKICHANGIA HOJA NA KUULIZA MASWALI
WALIOSHIRIKI MAFUNZO YALIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA FM HOTEL NJOMBE
WASHIRIKI WAKIWA KATIKA KAZI ZA MAKUNDI
Abiud Gamba Ni Mratibu Wa Mradi Wa Afrikani Conservation Tillage Network {ACTN}
MGENI RASMI NA MKURUGENZI MTENDAJI WA ACT AFRIKAN CONSERVATION TILLAGE NETWORK SAID MKOMWA AKITOA HOTUBA YAKE WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO YA SIKU NNE KWA WAKULIMA HAO.
MGENI RASMI NA MKURUGENZI MTENDAJI WA ACT AFRIKAN CONSERVATION TILLAGE NETWORK SAID MKOMWA AKITOA HOTUBA YAKE WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO YA SIKU NNE KWA WAKULIMA HAO.
Wakulima Wa Kutoka Mikoa Ya Iringa,Njombe Na Ruvuma Leo Wamehitimisha Semina Ya Siku Nne Kwa Kupewa Masharti Ya Kwenda Kuwaelimisha Wakulima Wengine Ambao Hawajahudhuria Semina Hiyo Ili Kudumisha Kilimo Hifadhi Kwa Manufaa Yao Na Taifa Kwa Ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La ACT Said Komwa Amesema Wa wakilishi Wa Wakulima Kutoka Mikoa Ya Nyanda Za Juu Kusini Wanatakiwa Kutumia Kilimo HifadhiKi Kitakacho wapatia Mazao Yakutosha Pasipo Kuharibu Udongo Na Kupanda Mazao Mzunguko.
Aidha Bwana Komwa Amesema Matumizi Ya Trekta Na Jembe La Kukokotwa Na Wanyama Inasababisha Kuharibu Ardhi Ambayo Hata Mkulima Akiweka Pembejeo Za Mborea Haitafanya Kazi Ipasavyo Na Hivyo Wanatakiwa Kutumia Kilimo Hifadhi Kwa Kutumia Masalia Ya Mimea.
Kwa Upande Wao Wakufunzi Wa Mafunzo Hayo Deogratias Ngotio Na Abiud Gamba Wameshauri Wakulima Waliopatiwa Mafunzo Hayo Kwenda Kuwaelimisha Ambao Hawajahudhuria Mafunzo Hayo Na Kuwa Makini Matumizi Ya Viwatilifu AMbavyo Vina Madhara Kwa Watumiaji.
Aidha Wakufunzi Hao Wamesema Kuwa Serikali Inapaswa Kusambaza Wataalamu Wa Kilimo Katika Maeneo Ambako Wakulima Wanapatikana Ili Kutengeneza Mashamba Darasa Na Kuwa Mfano Kwa Wakulima Wengine Na Kuiga Kilimo Hifadhi Kwa Manufaa Yao.
Wakizungumza Washiriki Wa Semina Hiyo Wamepongeza Kwa Elimu Iliyotolewa Kwa Siku Nne Mjini Njombe Ambapo Wameelezea Changamoto Zinazowakabili Katika Kilimo Ikiwa Ni Pamoja Na Kukosa Soko La Mazao Wanayozarisha Kwa Maeneo Ya Ludewa Na Songea.
Miongoni Mwa Changamoto Zinazowakabili Wakulima Hao Ni Pamoja Na Kukosekana Kwa Soko La Mahindi,Kulima Kilimo Cha Mazoea Na Ufugaji ,Huku Wakulima Wa Wilaya Ya Ludewa Wakisema Katika Wilaya Hiyo Vitendo Vya Rushwa Hufanyika Ili Waweze Kuuza Mazao Yao.
Semina Hiyo Ya Siku Nne Iliyotolewa Na Shirika La Afrikani Conservation Tillage Network Imeelezwa Kuwa Na Mafanikio Makubwa Kwa Wakulima Hao Endapo Watakwenda Kutekeleza Walioagizwa Ya Kwenda Kufundisha Wakulima Wengine Kutumia Kilimo Hifadhi.
No comments:
Post a Comment