WAZEE WA YAKOBI WILAYANI NJOMBE WANUFAIKA NA MIKOPO YA MBUZI NA KUKU KUTOKA SHIRIKA LA PADI
HAWA NI WAZEE WA KATA YA MTWANGO WAKIFURAHIA MIKOPO YA MBUZI ILIYOTOLEWA NA SHIRIKA LA PADI
MBUZI WANAOTOLEWA KWA WAZEE NA SHIRIKA LA PADI
HAWA NI WAWAKILISHI WA WAZEE WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE NA WANGING'OMBE
MWENYEKITI WA WAZEE POSTA KATI PIA NI MWAAKILISHI WA WAZEE WA WILAYA YA NJOMBE NA WANGING'OMBE BWANA ANDREW MHAGAMA
MRATIBU SHIRIKA LA PAD MKOA WA NJOMBE BI.RACHEL STEPHAN AKIWA OFISINI KWAKE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO
OFISI YA SHIRIKA LISILO KUWA LA SERIKALI MKOA WA NJOMBE LA PADI ILIYOPO MTAA WA CHAUGINGI
NA MICHAEL NGILANGWA -NJOMBE
Wawakilishi Wa Baraza La Wazee Katika Halmashauri Nne Za Wilaya Ya Njombe Na Wanging'ombe Wamelazimika Kutembelea Ofisi Za Wakurugernzi Wa Halmashauri Hizo Ili Kutambua Namna Huduma Za Matibabu Zinavyotolewa Kwa Wazee Katika Hospitali, Vituo Vya Afya Na Zahanati .
Akizungumza Na Uplands Fm Mwenyekiti Wa Wazee Katika Mtaa Wa Posta Kati Na Muwakilishi Wa Wazee Kwa Halmashauri Nne Za Wilaya Ya Njombe Na Wanging'ombe Bwana Andrew Mhagama Amesema Kuwa Lengo Kubwa La Kutembelea Ofisi Za Viongozi Hao Ni Kutaka Kufahamu Utaratibu Na Hatua Zinazochukuliwa Kwa Baadhi Ya Watumishi Wa Afya Wanaotumia Kauli Mbaya Kwa Wazee Wanapokwenda Kupatiwa Matibabu.
Aidha Bwana Mhagama Amesema Kuwa Kumekuwa Na Baadhi Ya Wazee Ambao Wanapoteza Maisha Kutokana Na Kukosa Matibabu Ambapo Amepongeza Kwa Ushirikiano Mkubwa Uliooneshwa Na Wakuu Wa Idara Na Wakurugenzi Wa Halmashauri Zote Mbili Pamoja Na Katibu Tawala Mkoa Wa Njombe Huku Akisema Kuwa Utekelezaji Wa Sera Ya Matibabu Bure Kwa Wazee Bado Haujapewa Kipaumbele.
Kwa Upande Wao Wajumbe Na Wawakilishi Wa Wazee Wilaya Ya Njombe Na Wanging'ombe Pamoja Na Kupongeza Serikali Kwa Kuunga Mkono Sera Ya Kuwapatia Wazee Matibabu Bure Katika Hospitali Pia Wamesema Kuwa Kunachangamoto Mbalimbali Ambazo Zimekuwa Zikiwakabili Ikiwemo Kukosekana Kwa Dawa Kwenye Hospitali,Vituo Vya Afya Na Zahanati Na Kusababisha Kwenda Kuzinunua Kwenye Maduka Binafsi.
Wamesema Baraza La Wazee Linawaunganisha Wazee Wote Kujua Na Kuweza Kudai Haki Zao Ambapo Wameomba Wazee Kujiunga Kwenye Baraza Hilo La Wazee Ili Kujua Haki Zao Katika Maeneo Mbalimbali Huku Wakilishukuru Shirika Lisilo La Kiserikali La PADI Kwa Kuwasaidia Kuwapatia Misaada Ikiwemo Kuhamasisha Wazee Kuungana Na Kupatiwa Matibabu Bure Kama Sera Ya Serikali Inavyo Sema.
Kwa Mujibu Wa Senza Ya Mwaka 2012 Halmashauri Ya Mji Wa jombe Inakadiliwa Kuwa Na Wazee 7423,Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Ikiwa Na Wazee 4888,Makambako Wazee 5348 Na Halmashauri Ya Wilaya Ya Wanging'ombe Ikiwa Na Wazee 9224 Ambao Wote Wanastahili Kupatiwa Matibabu Bure.
No comments:
Post a Comment