Thursday, May 14, 2015
WAUGUZI NJOMBE WAUNGANA NA WAUGUZI WENGINE DUNIANI KOTE KUADHIMISHA SKUKUU YAO
WAUGUZI WAKITOA BURUDANI YA MAIGIZO KWA MGEN RASMI
TUMAIN MPONJI AKISOMA RISALA KWA MGENI RASMI
MGENI RASMI AKIKABIDHIWA RISALA YA WAUGUZI
MC JIMMY NGUMBUKE AKITANGAZA UTARATIBU
Katika Kuadhimisha Siku Ya Wauguzi Duniani Serikali Imeombwa Kutatua Baadhi Ya Changamoto Mbalimbali Zinazowakabili Watumishi Wa Umma Hususani Wauguzi Ikiwemo Mishahara Na Kuboreshewa Mazingira Ya Kufanyia Kazi Pamoja Na Kuongeza Vitendea Kazi Na Dawa Kwenye Maeneo Ya Kutolea Huduma Za Afya.
Hayo Yamebainishwa Kwenye Maadhimisho Ya Siku Ya Wauguzi Duniani Ambayo Kwa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Yalifanyikia Katika Ukumbi Wa Day To Day Kibena Yakiwakutanisha Wauguzi Wa Afya Waliopo Maeneo Mbalimbali Ya Halmashauri Hiyo Wakiwemo Wa Mijini Na Vijijini.
Akizungumza Kwa Niaba Ya Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe B.Iluminata Mwenda Akiwa Mgeni Rasmi ,Afisa Utumishi Wa Halmashauri Hiyo Bwana Gualbert Mbujilo Amesema Kuwa Kanuni Ya Utumishi Wa Umma Ya Mwaka 2003 Kifungu Cha 1003 Sekisheni Ndogo Ya Kwanza Na Ya Pili Inasema Mwajili Anatakiwa Kutengeneza Mpango Wa Mafunzo Wa Kila Mwaka Kwa Watumishi Wake.
Aidha Bwana Mbujilo Amesema Kuwa Mwajili Ana haki Ya Kuwawezesha Baadhi Ya Watumishi Kwenda Kusoma Kutokana Wakuu Wa Idara Wa Halmashauri Kusahau Majukumu Yao Na Kwamba Kila Mwaka Mkuu Wa Idara Anatakiwa Kutenga Fungu La Fedha Kwaajili Ya Kuwasaidia Wale Wanaokwenda Kusoma Huku Akiwaomba Wafanyakazi Kupeleka Gharama Mapema Kwani Kusoma Ni Haki Ya Kila Mtumishi.
Amesema Kuwa Mtumishi Ambaye Amejiendeleza Kimasomo Anatakiwa Kupandishwa Cheo Mara Moja Na Kuwataka Watumishi Kuanzia Sasa Watakaokwenda Kusoma Wafike Katika Ofisi Ya Utumishi Ili Kutatuliwa Matatizo Yanayowakabili Ikiwemo Ya Mishahara,Kupandeshwa Vyeo Kwa Waliojiendeleza Na Matatizo Mbalimbali Ya Kiutumishi.
Astrida Mwingira Ni Mwenyekiti Msaidizi Wa Chama Cha Wauguzi Mkoa Wa Njombe TANA Amesema Kuwa Wauguzi Wanakabiliwa Na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Baadhi Ya Wauguzi Kuwa Wachache Katika Kuchangia Maadhimisho Hayo Kwa Kutotambua Umuhimu Wake Ambapo Ombi Kubwa Kwa Mwajili Wao Kutenga Fungu Kwaajili Ya Sherehe Hizo Huku Yalioandikwa Kwenye Lisala Mwajili Akitakiwa Kutatua Kwa Wakati.
Katika Risala Yao Iliyosomwa Na Tumain Mponji Imeomba Kujengwa Kwa Uzio Kuzunguka Hospitali Ya Kibena Kwaajili Ya Usalama Wa Wagonjwa Na Wauguzi ,Mhasibu Kuwa Na Fedha Ya Kununulia Vifaa Tiba Vya Dharula Pamoja Na Kupunguza Urasimu Wa Kuidhinisha Fedha Ya Kununulia Vifaa Tiba.
Kauli Mbiu Ya Maadhimisho Hayo Ambayo Imefanyika Mei 12 Inasema, NGUVU YA MABADILIKO KATIKA KUFIKIA UTOAJI WA HUDUMA BORA,RAHISI,YENYE TIJA NA INAYOPATIKANA KWA WOTE{ A FORCE FOR CHANGE,CARE EFFECTIVE ,LOST EFFECTIVE}.
Na Michael Ngilangwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment