Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, May 14, 2015

TAIFA STARS YAWASILI RUSTENBURG AFRIKA KUSINI


thumb_IMG_0771_1024
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mara baada ya kwasili  leo mchana majira ya saa 6 kamili katika jiji la Rustenburg nchini Afrika Kusini.
thumb_IMG_0774_1024
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mara wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili nchini Afrika Kusini.
…………………………………………………………………………………….
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili leo mchana majira ya saa 6 kamili katika jiji la Rustenburg na kufikia katika hoteli ya Hunters Rest – Protea iliyoypo pembeni kidogo ya  jiji.
Taifa Stars ambayo iliondoka jana joni jijini Dar es salaam jijini Dar es salaam na kufika OR Tambo saa 5 usiku, ilipata mapokezi mazuri kutoka kwa waandaji wa michuano ya COSAFA pamoja na watanzania wanaoishi jijini humo, ililala katika hoteli ya Southern Sun.
Safari ya kutoka Johannesburg kuelekea Rustenburg ilichukua takribani masaa mawili na msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF Ephaphra Swai.
Wachezaji waliopo na timu Rutsenburg ni Deogratius Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Salim Mbonde, Aggrey Moriss, Joram Mgeveke, Said Juma, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto, Ibhrami Ajib, Juma Luizio, John Bocco, Mrisho Ngasa na Saimon Msuva.
Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kufanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Rustenburg Impala Bowling Club majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Kusini sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment