Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, May 13, 2015

RAIS WA BURUNDI APINDULIWA KIJESHI.

 
Aliyekuwa Rais wa Nchi ya Burundi Pierre Nkurunzinza
 
Baada ya vuta ni kuvute  ya wiki kadhaa ya wananchi Nchini  Burundi  na jeshi la nchi hiyo hatimaye Rais ambaye ndiye aliyekuwa chanzo cha migongano hiyo ametangazwa kupinduliwa.
Kwa mujibu wa taarifa  kutoka Bujumbura mji mkuu wa Nchi hiyo  zinasema kuwa ,  Meja Jenerali Godefroid Niyombareh  ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi.
Meja Jenerali Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi na itakayoitawala nchi hiyo kwa kipindi cha mpito.
Kwa mujibu wa taarifa  iliyopeperushwa vyombo vya habari  Nchini humo Jeshi limesema limechukua hatua hiyo  baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kuandamana kupinga awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza..
Akiyazungumza hayo Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi na inaelezwa kuwa Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Rais Nkurunzinza alipuuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo mapendekezo yaliyotolewa na mataifa rafiki kwa lengo la kutatua mgogoro uliolikumba taifa hilo.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''

Hatua ambayo imekuja ikiwa  Viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wanaketi  hii leo mjini Dar es Salaam kujadili mbinu za kutatua mgogoro wa kisiasa, mkutano  uliochini mwenyekiti jumuiya ya Afrika ya mashariki  Rais  Jakaya Kikwete, aliyeuitisha baada ya ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jumuiya hiyo, kwenda Bujumbura wiki iliyopita.

Maelfu ya wanaburundi wameikimbia nchi yao kwenda nchini ikiwamo Tanzania huku zaidi ya Raia 20 wakiyapoteza maisha yao  tangu April 26  kuanza kwa maandamano ya kupinga uamuzi wa Rais Nkurunzinza kugombea mhura wa tatu wa Urais.
Nkurunzinza aliyeingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2005 akimpokea Domitien Ndayizeye kwa kuchaguliwa na bunge kuiongoza nchi hiyo na alifanikiwa kushinda uchaguzi wa mwaka 2010 lakini  tukio lilioonekana kupingwa na wananchi wake ni kuwania awamu ya tatu kinyume ya katiba. 
 
Kwa Hisani Ya James Hfesto Blog
 
 'Serikali ya Pierre Nkurunziza imepinduliwa Burundi'
 
 
Mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Burundi ametangaza kuwa Rais Pierre Nkurunziza amepinduliwa baada ya machafuko ya zaidi ya wiki mbili yaliyozuka baada ya Nkurunziza kuamua kugombea urais kwa muhula wa tatu mfululizo.

Meja Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza leo kupitia redio ya taifa jijini Bujumbura kwamba, kuanzia sasa Rais Pierre Nkurunziza si rais tena wa Burundi. Amesema, serikali imevunjwa, makatibu wa kudumu wa mawaziri wataendesha masuala ya nchi hiyo hadi tangazo jingine litakapotolewa.

Tangazo la Meja Jenerali Niyombare limekuja baada ya jeshi la Burundi kuzizingira ofisi za redio ya taifa katika jiji la Bujumbura.

Mapema leo polisi wa Burundi wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji waliojaribu kulivamia bunge.
Baada ya kutangazwa habari hiyo, ofisi ya Rais Nkurunziza imeandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa jaribio hilo la mapinduzi limeshindwa.

"Hali ya mambo imedhibitiwa, hakuna mapinduzi nchini Burundi," umesema ujumbe huo.
 
Kwa Hisan Ya Idhaa Ya Kiswahili Ya Radio Tehran.

No comments:

Post a Comment