Tuesday, May 26, 2015
MH.MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA NJOMBE DKT PINDI HAZARA CHANA AHAMASISHA BIMA YA AFYA KWA JAMII
MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA NJOMBE DKT PINDI HAZARA CHANA
Mbunge Wa Viti Maalumu Mkoa Wa Njombe Na Naibu Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii,Wanawake,Njinsia Na Watoto Dkt Pindi Hazara Chana Amewataka Wananchi Kujiunga Na Mfuko Wa Bima Ya Afya Kwa Kuchangia Fedha Shilingi Elfu Kumi Kwaajili Ya Matibabu Katika Hospitali,Vituo Vya Afya Na Zahanati Kwa Manufaa Yao.
Rai Hiyo Imetolewa Na Mbunge Huyo Dkt Chana Wakati Akizungumza Na Mtandao Huu Kuhusiana Na Watanzania Kujiunga Na Mfuko Wa Bima Ya Afya Kwani Inaonesha Bado Hawaja Tambua Umuhimu Wa Mfuko Huo.
Aidha Dkt Chana Amesema Kuwa Ni Asilimia 20 Tu Ya Watanzania Ambao Wamejiunga Kwenye Mfuko Wa Bima Ya Afya Ukiacha Watumishi Wa Serikali Na Taasisi Mbalimbali Za Serikali Na Watu Binafsi Jambo Ambalo Linasababisha Kugharamia Matibabu Badala Ya Kwenda Kupata Huduma Hiyo Bule.
Dkt Chana Ametumia Fursa Hiyo Kuzungumzia Semina Ya Siku Moja Ambayo Inatarajia Kutolewa Mnamo Mei 26 Katika Ukumbi Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Ambayo Inalenga Kuongeza Uelewa Wa Kujiunga Kwenye Mfuko Wa Bima Ya Afya Kutoka Mfuko Wa Afya Ya Jamii.
Amesema Kuwa Semina Hiyo Inawalenga Wawakilishi Wa Wananchi Kutoka Kila Kata Katika Wilaya Ya Njombe Ambao Watakwenda Kutoa Elimu Hiyo Kwa Wananchi Vijiji Juu Ya Kujiunga Kwenye Mfuko Huo Na Faida Zake Ili Kupatiwa Matibabu Bure Kwa Waliochangia Shilingi Elfu 10 Kwa Mwaka Badala Ya Kulipia Fedha Kila Mgonjwa Anapokwenda Kwenye Huduma Ya Matibabu.
Kwa Upande Wao Baadhi Ya Wananchi Mkoani Njombe Wamekuwa Na Mtazamo Tofauti Kuhusiana Na Kujiunga Na Mfuko Huo Wa Bima Ya Afya Kwa Kusema Kuwa Hawaoni Umuhimu Wa Kuchangia Mfuko Wa Bima Ya Afya Ikiwa Katika Hospitali, Vituo Vya Afya Na Zahanati Hakuna Uhakika Wa Kupata Matibabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment