Saturday, May 23, 2015
HATIMAYE MAZISHI YA BASIL MWALONGO AMBAYE AMEDAIWA KUUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WANAOSADIKIKA KUWA NI ASKALI POLISI YAMEFANYIKA JANA MEI 22 KIJIJINI KWAKE LUGENGE WILAYANI NJOMBE
HUYU NI BASIL MWALONGO ENZI ZA UHAI WAKE NA MAZISHI YAKE YAMEFANYIKA JANA MEI 22 BAADA YA KUPIGWA RISASI NA WATU WANAODAIWA KUWA NI ASKALI POLISI KATIKA TUKIO LILILOTOKEA MEI 19 KATIKA KIRABU CHA NYONDO MTAA WA KAMPALAGE HUKU MMOJA AKIJERUHIWA AMBAYE NI FRED SANGA
HIZI NI BAADHI TU YA RISASI ZILIZOTUMIKA KUMUULIA MAREHEMU BASIL MWALONGO NA KUJERUHI MMOJA FRED SANGA NA AMBAZO HAZIJATUMIKA ZILIZOKUTWA ENEO LA TUKIO
HIKI NI KIBAL AMBACHO WANANCHI WAMEKUBALI KUKIPOKEA NA KUFANIKIWA KUZIKA BAADA YA KIBALI CHA KWANZA KUKATALIWA
HAWA NI WANANCHI WAKIWA KWENYE MAZISHI YA MAREHEMU BASIL MWALONGO WAKIWA KIJIJINI LUGENGE.
HILI NI KABURI AMBALO AMEZIKWA MAREHEMU BASIL MWALONGO ALIYEUWAWA KWA KUPIGWA RISASI
MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO LA NJOMBE KUSINI ALLY MHAGAMA MAARUFU KAMA DR.SAGASAGA AKITUPIA MCHANGA KWENYE KABURI LA KIJANA BASIL MWALONGO AMESHIRIKI MAZISHI HAYO.
KATEKISTA WA KANISA KATHOLIKI AKIONGOZA IBADA YA MAZISHI YA KIJANA BASIL MWALONGO KATIKA KIJIJI CHA LUGENGE
OBADIA CHOGA NI MWENYEKITI WA MTAA WA MGENDELA KATA YA NJOMBE MJINI AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI AGREY MTAMBO AKIWA KWENYE MAKABURI YA KIJIJI CHA LUGENGE ALIKOZIKWA MAREHEMU BASIL MWALONGO ALIPIGWA RISASI NA WATU WANAOSADIKIKA KUWA NI ASKALI POLISI.
MSHAURI WA MGAMBO WILAYA YA NJOMBE AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA NJOMBE BWANA LEONALD MWAJOMBE AKIWA KWENYE MAKABURI ALIKO ZIKWA MAREHEMU HUYO.
MAMA WA MAREHEMU BASIL MWALONGO AKIWA KWENYE ENEO LA MAZISHI KIJIJINI LUGENGE
HAPA KABURI TAYARI LIMEKWISHA KAMILIKA NA MAREHEMU KASHA ZIKWA NA WANANCHI WANAONDOKA KUELEKEA NYUMBANI KWAO
HAPA WANANCHI WANARUDI NYUMBANI KWAO BAADA YA MAZISHI HAYO
HUYU NI DIWANI WA KATA YA LUPONDE STAMIUS MAYEMBA HAPA ANARUDI NDO ANATOKA MAKABURINI KWA MAREHEMU BASIL MWALONGO
HAPA NI NYUMBANI KWA WAZAZI WA MAREHEMU BASIL MWALONGO
Hatimaye Mazishi Ya Marehemu Basil Mwalongo Ambaye Ameuwawa Na Watu Wanaodaiwa Kuwa Ni Askali Polisi Katika Kilabu Cha Nyondo Mtaa Wa Kampalage Yamefanyika Leo Kijijini Kwao Lugenge Baada Ya Wananchi Na Ndugu Wa Marehemu Kukubaliana Na Kibali Cha Pili Walichokwenda Kuchukua Katika Hospitali Ya Kibena Kutokana Na Kibali Cha Kwanza Kukataliwa.
Akizungumza Kwenye Mazishi Hayo Kwa Niaba Ya Mwenyekiti Wa Kamati Ya Ulinzi Na Usalama Wilaya Ya Njombe Mshauri Wa Mgambo Wilaya Bwana Leonad Mwajombe Amesema Kuwa Serikali Inalaani Vikali Kitendo Cha Polisi Mkoa Wa Njombe Kuuwa Raia Si Cha Busara Na Kwamba Watahakikisha Hatua Kali Zinachukuliwa Kwa Waliohusika Na Tukio Hilo .
Aidha Bwana Mwajombe Amesema Kuwa Tukio Hilo Limeishtua Serikali Mkoani Njombe Na Kusema Kuwa Serikali Inatoa Pole Kwa Waliokutwa Na Msiba Huo Wa Kuondokewa Na Ndugu Huyo Na Kwamba Inakusudia Kupata Ukweli Pasipo Matatizo Yoyote Na Kuwaondoa Hofu Juu Ya Kupatikana Kwa Haki Katika Tukio Hilo.
Diwani Wa Kata Ya Lugenge Bwana Filoteus Mligo Ametupia Lawama Viongozi Wa Serikali Kwa Kushindwa Kushiriki Kikamilifu Katika Kuuzika Mwili Wa Marehemu Huyo Na Kwamba Mwili Huo Ulitelekezwa Kwenye Nyumba Ya Wanandugu Na Wao Kuondoka Pasipo Taarifa Zozote Jambo Ambalo Limeleta Simanzi Kubwa Kwa Wananchi Na Viongozi Wa Kata Hiyo.
Akizungumza Kwa Niaba Ya Diwani Wa Kata Ya Njombe Mjini Agrey Mtambo,Mwenyekiti Wa Mtaa Wa Mgendela Bwana Obadia Choga Amelaani Kitendo Cha Kuuwawa Kwa Kijana Huyo Kwa Risasi Na Kusema Kuwa Jeshi La Polisi Limetumia Nguvu Kubwa Mno Katika Kuimarisha Usalama Wake Kwa Wananchi Hadi Kufikia Hatua Ya Kumpiga Risasi Kijana Huyo Ambaye Hakuwa Na Kosa Lolote Huku Akisema Kata Ya Njombe Mjini Itaendelea Kuwa Jirani Na Ndugu Wa Marehemu Katika Kutafuta Haki Zao.
Leo Mei 22 Ni Siku Ya Tatu Tangu Kutokea Kwa Tukio La Mauaji Ya Kijana Basil Mwalongo Huku Majeruhi Fred Sanga Akiendelea Na Matibabu Lakini Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Bado Halijatoa Tamko Lolote La Kuwashikilia Waliohusika Na Mauaji Hayo Na Chanzo Chake Licha Ya Waandishi Wa Habari Kwenda Ofisini Kwake Kupata Tamko La Tukio Hilo.
Mnamo Tarehe 27 Mwezi Februari Mwaka 2013 Askali Wa Polisi Makete Mkoani Njombe Walituhumiwa Kumuua Mwalimu Sote Kawamba Na Kupoteza Maisha Wakati Akitoa Fedha Kwenye ATM Mashine Ya Benk Ya NMB Baada Ya Kupigwa Na Risasi Mgongoni, Huku Wilaya Ya Ludewa Mnamo Tarehe 23 Mwezi January Mwaka Huu Kijana Mmoja January Mtitu Miaka 20 Aliuwawa Na Askali Polisi Kwa Kupigwa Risasi Akiwa Eneo La Mdonga Ludewa Mjini Mkoani Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment