BAADHI YA VIONJGOZI WA KIJIJI CHA ITAMBO PAMOJA NA WANANCHI WA KIJIJI HICHO WAKIWA KWENYE ZOEZI LA UWEKAJI JIWE LA MSINGI
MHANDIS WA MAJI WILAYA YA NJOMBE WA UPANDE WA KULIA MWENYE SUTI NYEUSI SENGAYAVENE MKALIMOTO
WAZEE WA KIJIJI CHA ITAMBO WAKIWA NA FURAHA KUBWA BAADA YA KUPATA MAJI
Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi.Sarah Dumba Ameweka Jiwe La Msingi Kwenye Mradi Wa Maji Unaotekelezwa Na Shirika La Walemavu Nyombo Kwa Kushirikiana Na Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Pamoja Na Wananchi Wa Kijiji Cha Itambo Wenye Zaidi Ya Shilingi Milioni Mia Mbili Hadi Kukamilika Kwake.
Akizungumza Na Wananchi Wakati Wa Kuweka Jiwe La Msingi Kwa Niaba Ya Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Kaimu Katibu Tawala Wa Wilaya Bi.Anna Wikatye Amesema Kuwa Mradi Huo Uliowekewa Jiwe La Msingi Ni Ukombozi Kwa Wakazi Wa Kijiji Cha Itambo Kupata Maji Kwa Umbali Usiyozidi Mita 400 Kwa Mujibu Wa Sera Ya Maji Ya Taifa Ya Mwaka 2002.
Aidha Bi.Wiketye Amesema Kuwa Kukamilika Kwa Mradi Huo Kutasaidia Kupunguza Muda Mwingi Uliokuwa Ukipotea Kwa Akina Mama Kuyafuata Maji Kwenye Milima Na Mambonde Ambayo Siyo Safi Na Salama Ambapo Kwa Sasa Wananchi Watashiriki Kikamilifu Katika Uzarishaji Mali Na Kukuza Uchumi Wa Kila Mmoja.
Kaimu Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Ambaye Ni Mhandis Wa Maji Sengayavene Mkalimoto Pamoja Na Kuwapongeza Wananchi Kwa Kuunga Mkono Jitihada Za Serikali Na Shirika La Walemavu Nyombo Kupitia Wafadhili Kutoka Hispani Wa Manos Unidas Katika Kuwafikishia Maji Lakini Pia Amesema Wananchi Wamechangia Zaidi Ya Milion 34, Halmashauri Imechangia Zaidi Ya Milioni 50 Huku Shirika Hilo Likiwa Limepeleka Zaidi Ya Shilingi Milioni Mia 119 Kukamilisha Mradi Huo.
Emmanuel Haule Ni Katibu Wa Shirika La Walemavu Nyombo Akisoma Risala Fupi Ya Utekelezaji Wa Mradi Huo Amesema Hadi Sasa Shirika Limekamilisha Shughuli Za Ujenzi Wa Inteki,Njia Kuu Yenye Urefu Wa Kilomita 10.9,Chemba Za Valvu,Wash Out Na Tenki Moja La Lita elfu 45000 Ambapo Kwa Sasa Wanatengemea Kuendelea Na Ujenzi Wa Tenki La Pili,Njia Za Kusambaza Maji Kilomita 5.1 Pamoja Na Jumla Ya Vituo Vya Bomba 19.
Kwa Upande Wao Wananchi Wa Kijiji Cha Itambo Kata Ya Mfriga Wameshukuru Shirika La Walemavu Nyombo Kuwasaidia Kupeleka Maji Kwa Kushirikiana Na Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Ambapo Wamesema Kwa Muda Mrefu Hawajawahi Kupata Maji Hayo Tangu Kuanzishwa Kwa Kijiji Hicho Na Kupata Hati Ya Usajili Wake Mwaka 1974 Akina Mama Hutegemea Maji Ya Mabondeni.
Mradi Huo Umewekewa Jiwe La Msingi Ikiwa Ni Kutekeleza Sera Ya Maji Ya Taifa Ya Mwaka 2002 Ya Kuwafikishia Huduma Hiyo Kwa Wananchi Vijijini Ambapo Katika Wiki La Maji Ambalo Kilele Chake Kilifanyika Machi 22 Mwaka Huu Yakiwa Na Kauli Mbiu Isemayo Maji Kwa Maendeleo Endelevu Ambayo Inatokana Na Kauli Mbiu Ya Siku Ya Maji Duniani Ya Mwaka 2015 Na Kwamba Bila Maji Hakuna Maendeleo.
No comments:
Post a Comment