Monday, March 16, 2015
ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA LIMEANZA LEO KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE KWA KATA TATU BAADA YA KUHITIMISHA HALMASHAURI YA MAKAMBAKO
Wakati Zoezi la Uandikishaji Kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Likiwa Limeanza Kwa Kata Tatu za Halmashauri ya Mji wa Njombe , Baadhi ya Changamoto Zimejitiokeza Kwa Baadhi ya Vituo Ikiwemo Kasi Ndogo ya Uandikishaji Kwa Wataalam.
Aidha Changamoto Nyingine Zilizojitokeza Katika Zoezi Hilo ni Pamoja na Baadhi ya Mashine Kufanya Kazi Taratibu na Kutumia Zaidi ya Dakika 10 Kuandikisha Mtu Mmoja,Huku Kituo cha Mpechi Kionesha Mkanganyika wa Kata Gani Kipo.
Mwandishi Wa Mtandao Huu Ametembelea Baadhi ya Vituo Hivyo Kujionea Zoezi Zima Linavyokwenda na Kufanikiwa Kuzungumza na Wananchi Kuhusiana na Zoezi Hilo na Kuelezea Changamoto Walizokutana Nazo , Kama Wanavyoeleza.
Mapema Asubuhi ya Leo Wananchi Wamejitokeza Kwa Wingi Kwenye Vituo Vya Kujiandikishia Huku Wakiomba Muda wa Kujiandikisha Kuongezwa Ili Wananchi Wote Wenye Sifa za Kujiandisha Waandikishwe
Akizungumza Kwa Upande Wake Diwani Wa Kata Ya Mjimwema Jimmy Ngumbuke Amesema Kuwa Pamoja Na Kuwa Zoezi Hilo Linaonekana Kwenda Taratibu Kwa Baadhi Ya Vituo Lakini Amesema Linakwenda Vizuri Na Kuwataka Wananchi Kuendelea Kujitokeza Kujiandikisha Kwaajili Ya Kupata Vitambulisho Vitakavyo Wasaidia Kupiga Kura ifikapo 0ctober Mwaka Huu.
Kata Tatu Zimeanza Kujiandikisha Ikiwemo Kifanya,Yakobi Na Mjimwema Ambapo Kwa Kiasi Kikubwa Zoezi Hilo Limeonekana Kufanikiwa Licha Ya Kuwepo Kwa Changamoto Ndogondogo.
Aidha Zoezi Hilo Pia Limeanza Kwa Baadhi ya Kata za Wilaya za Makete , Wanging'ombe na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.
............................................................................................
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment