Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, November 24, 2014

WAKULIMA WA NJOMBE WA PELEKEA SOKO LA MAHINDI

Afisa Ushirika Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Thomas Nyamba  Ametolea Ufafanuzi Kuhusiana  Na Kufufuliwa Kwa Chama Cha Ushirika  Cha Mkoa Wa Njombe Ambacho Hapo Awali Kilikuwa  Kikiitwa NJOLUMA Ambapo  Kwa Sasa Kinaitwa Chama Cha Ushirika Cha Mkoa Wa Njombe.

Akizungumza  Afisa Ushirika Huyo Bwana Nyamba Amesema Kuwa Chama Kikuu Cha Ushirika Cha Mkoa Wa Njombe  Kitakuwa Kinahudumia Halmashauri Zote Sita Za Mkoa Wa Njombe Ambapo Kwa Kuanza Chama Hicho Kimeanza Kutafuta Fedha Kwaajili Ya Kuanza Zoezi La Kununua Mahindi Kutoka Kwa Wakulima.

Bwana Nyamba Amesema Kuwa Kila  Halmashauri Inayolima Mahindi Imewekewa Kituo Cha Kukusanyia Mahindi  Isipokuwa  Wilaya Ya Makete   Na Kwamba Kwa Wilaya Ya Njombe Kituo Cha Kukusanyia Mahindi Kipo Matembwe,Nyombo Na Ninga.

Amesema Kuwa Halmashauri Ya Wilaya Ya Ludewa Kituo Kitakuwepo Mlangali ,Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kituo Kitakuwa Luponde,Halmashauri Ya Mji Wa Makambako Kituo Kipo Kwenye Chama Cha Msingi  Cha Makambako  Na Wanging'ombe Kipo Mambegu Ambavyo Vituo Hivyo Vitakusanya Mahindi Kwa Maeneo Yanayovizunguka Yote.

Bwana Nyamba Amesema Kuwa Chama Kikuu Cha Ushirika Cha Mkoa Wa Njombe Kimefanikiwa Kupata Mkopo Toka Benk Ya CRDB  Wa Shilingi Milioni Mia Nne Ambao Unasaidia Kununua Mahindi Kutoka Kwa Wakulima Ambapo Mkopo Huo Hautosherezi Matakwa  Ya Kununua Mahindi Kwa Wingi.


Aidha Bwana Nyamba Ametoa Wito Kwa  Wakulima Kushikamana Ili Kukikuza Chama Hicho Ambapo Amesema Kubadilishwa Kwa Jina La Njoruma  Kumetokana na Changamoto Ambazo Chama Hicho Kilizipata  Hapo Awali  Na Wajumbe Wakaamua Kubadili Jina Hilo Lisiwepo Kabisha Badala Yake Liwepo La Chama Kikuu Cha Ushirika.



No comments:

Post a Comment