diwani wa kata ya makungu Mgololo Yohanis cosmas kaguo
KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN IRINGA
Diwani wa
kata ya Makungu Mgololo Yohanis cosmas kaguo amesema
tatizo la miundo mbinu katika
kata yake limepungua kwa asilimia kubwa
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz amesema kuwa amejitahidi
kutoa elimu kwa wananchi na kujenga majengo mbalimbali ya
kisasa katika shule za sekondari na shule za msingi.
kaguo ametaja
baadhi ya majengo waliojenga ni pamoja na madarasa ,vyoo,viwanja vya michezo
na kuzipa shule zote za eneo hilo vifaa vya michezo, ujenzi wanyumba za walimu pamoja na maabara
katika shule mbili za sekondari zizopo katika kata hiyo
Aidha kaguo amesema kuwa katika kata ya
makungu wametimiza lengo la rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania dr jakaya mrisho kikwete kwa kujenga
maabara katika shule zote mbili za kata hiyo kwa kujenga maabara zenye vyumba
vitatukwa kila sekondari vilivyo na
ubora wa kitaifa
Hivyo
kutimiza lengo la wanafunzi wa kata hilo kusoma huku wakiwa na maabara za
kisasa na zenye kiwango cha kitaifa na kuwafanya wanafunzi kusoma masomo ya
sayansi kwa kuwa maabara za kufanyia mazoezi katika masomo yao tayari
zimepatika na kuwaomba wanafunzi hao kusoma kwa juhudi masomo ya sayansi .
Pia diwani
kaguo amewashuku wananchi wa kata hiyo ya makungu iliyopo mgololo kwa kuitikia
wito wa ujenzi wa maabara na kushiriki katika kazi mbalimbali za kimaendeleo
ambapo wamempa moyo wa yeye kujituma zaidi na kuwatumikia wananchi katika
kuleta maendeleo.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment