Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, November 13, 2014

BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZ ASKOFU MSTAAFU WA NNE WA KKKT DAYOSISI YA KUSINI NJOMBE CLEOPA LUKILO AMEFARIKI DUNIA

Wa Kwanza Kushoto Aliyeshika Biblia ni Marehemu Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe Cleopa Lukilo Aliyefariki Ghafla Majira ya Saa Tisa Usiku wa Kuamkia Leo .Marehemu Askofu Cleopa Lukilo Enzi za Uhai Wake Kabla Hajastaafu Mwaka 2011
 
Na Gabriel Kilamlya NJOMBE

Askofu Mstaafu wa Nne wa KKKT  Dayosisi ya Kusini Njombe Cleopa Akutulaga Lukilo Amefariki Usiku wa Kuamkia Leo Akiwa Nyumbani Kwake Mtaa wa Nazareth Njombe.

Taarifa za Awali Zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Dayosisi Hiyo Mchungaji Timias Mhomisoli Kwa Niaba ya Askofu Mkuu Issaya Japhet Mengele Amesema Kuwa Kifo Hicho Kimetokea Majira ya Saa Tisa Usiku wa Kuamkia Leo.

Aidha Mhomisoli Amesema Kuwa Taarifa za Awali Zinasema Kifo Hicho ni Cha Ghafla na Huenda Kimetokana na Umri wa Miaka 65 Aliokuwa Nao.

Amesema Kuwa Askofu Huyo Mstaafu Alizaliwa Februari 13 Mwaka 1949 Ambapo Amekuwa Askofu wa Nne Tangu Mwaka 2004 Hadi 2011 Alipomuachia Askofu wa Sasa Issaya Japheth Mengele.

Hadi Sasa Mwili wa Marehemu Umepelekwa Kuhifadhiwa Katika Hospitali ya Misheni Ilembula Huku Uongozi wa Dayosisi Hiyo Ukiendelea na Vikao Kwa ajili ya Taratibu za Mazishi Yatakayofanyika Katika Kanisa Kuu la Dayosisi Hiyo.
 
Mtandao huu wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com Utaendelea Kukuletea Taarifa na Taratibu Nzima Juu ya Msiba Huo Kupitia Vipindi Vyetu.

Mungu Alitoa na Mungu Ametwa Jina La Bwana Lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment