WAAGWA WAKIREJEA UKUMBINI
MBUNGE NA NAIBU WAZIRI UJENZI GERSON HOSEA MALANGALILA LWENGE AKIKAGUA MAONESHO YA WANAFUNZI KATIKA SAYANSI
MKUU WA SHULE YA SEKONDARI PHILIP MANGULA GODFREY MWALONGO AKISOMA RISALA FUPI YA SHULE KWA MGENI RASMI
HAWA NI WAAGWA WAKISIKILIZA KWA UMAKINI HOTUBA YA MGENI RASMI
MGENI RASMI AKIKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE PHILIP MANGULA SEKONDARI
WATUMISHI NA VIONGOZI MBALIMBALI WA SHULE WAKIWA KTIKA PICHA YA PAMOJA NA MGENI RASMI
Na Michael Ngilangwa-Njombe
Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Gerson Hosea Malangalila Lwenge Amewaagiza madiwani wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanaingiza kwenye bajeti mpango wa kuanza ujenzi wa bwaro la chakula katika shule ya sekondari Philip Mangula Ambpo kukosekana kwa bwaro hilo imesababisha wanafunzi kulilia nje chakula.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi mbaye ni Naibu waziri wa Ujenzi Mhandis Gerson Lwenge wakati akiwa Mgeni Rasmi kwenye Mahafari ya saba ya Kidato cha Nne katika shule ya sekondari Philip Mangula kufuatia kukabiliwa na changamoto hiyo ya bwalo la chakula.
Gerson Lwenge pamoja na kuwataka Madiwani wa halmashauri hiyo kuweka bajeti na mikakati kwenye vikao vya baraza la madiwani ya kujenga bwalo la chakula katika shule hiyo pia amewataka wananchi wa kata ya Imalinyi na Kata nyingine za Taarafa ya Imalinyi kushiriki ujenzi huo kwa kuchangia michango ili kukamilisha mapema Ambapo pamoja na Mambo mengine Ameunga mkono kwa kuchangia shilingi milioni mbili za kuanzia ujenzi huo.
Aidha Mbunge huyo Gerson Lwenge pia ametoa msaada wa Vitabu 30 vya masomo mbalimbali vikiwemo vya sayansi Ambapo amesema changamoto ya kukosekana kwa walimu wa masomo ya sayansi ifikapo mwaka 2015 tatizo hilo litakuwa limekwisha kwani anakwenda kulifikisha wizarani ili kuongeza jitihada za kupeleka walimu wa masomo hayo kwa shule zote za sekondari.
Akitoa taarifa fupi mbele ya Mgeni rasmi Mkuu wa shule ya sekondari Philip Mangula bwana Godfrey Mwalongo amesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi,upungufu wa mabweni mawili,matundu 21 ya vyoo na nyumba 15 za walimu Jambo linalosababisha walimu kuishi nje na mahala pa kazi.
Katika risala fupi ya waagwa iliyosomwa na bi.Alumbwage Nyagawa imesema jumla ya wanafunzi 120 wanatarajia kufanya mitihani ya Kidato cha nne mwaka huu ikiwa walianza wakiwa wanafunzi 200 kutokana na sababu mbalimbali imesababisha kufikia idadi hiyo Ambapo kwa kipindi chote hicho wamekabiliwa na tatizo la kukosa walimu wa masomo ya sayansi ikiwemo fizikia na Hisabati.
Ziara ya Mbunge Na Naibu waziri wa Ujenzi Gerson Hosea Malangalila Lwenge hii leo inaendelea kwa vijiji vya kata ya Ilembula kukagua Maendeleo ya Mradi wa Umeme wa REA Ambao umeanza kutekelezwa katika kata hiyo.
No comments:
Post a Comment