Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, October 19, 2014

MBUNGE NJOMBE NA NAIBU WAZIRI UJENZI AKAGUA MRADI WA UMEME VIJIJI REA ILEMBULA NA UHAMBULE






 VIONGOZI MBLIMBALI WA SHIRIKA LA UMEME WANGING'OMBE NA KANDA YA KUSINI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MBUNGE KATIKA ENEO LA NGUZO ZA UMEME ILEMBULA




 NGUZO ZA UMEME  UNAOSAMBAZWA KWA WANANCHI VIOJIJINI REA KATA YA ILEMBULA

 wafanyalazi tanesco wanaofanya kazi ya kusimika nguzo za mradi wa umeme  vijijini REA











 MBUNGE HUYO AKIFUKIA KIFUSI KWENYE NGUZO KUWASAIDIA  MAFUNDI
 MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MAGHARIBI GERSON HOSEA MALANGALILA LWENGE  AKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WANANCHI WA VIJIJI VYA KANA MALENGA NA MWENYE SHATI NYEUPE NI MENEJA WA USAMBAZAJI WA MRADI WA UMEME VIJIJI  REA KANDA YA KUSINI KWA VIKOA YA NJOMBE,IRINGA,RUKWA,MBEYA NA KATAVI BI.SALOME NKONDORA




 MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MAGHARIBI GERSON HOSEA LWENGE AKIWA NA WANANCHI WA VIJIJI VYA WANGUTWA KATIKA PICHA YA PAMOJA ALIPO KUWA AMETEMBELEA JANA. Na Michael Ngilangwa -Njombe

Wananchi Wilayani Wang'ing'ombe Mkoani Njombe wametakiwa kuboresha nyumba zao ili  kuingiziwa mradi wa umeme Vijiji REA unaotarajia kuwanufaisha wananchi wa vijiji arobaini  vilivyopo kwenye mpango wa kufikishiwa  umeme huo  mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Ambaye ni Naibu waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge wakati akikagua utekelezaji wa Mradi wa kusambaza umeme Vijiji REA Wakati akizungumza na Baadhi ya Wananchi wa vijiji vya Kata za Ilembula na Uhambule.

Mbunge Gerson Lwenge amewataka wananchi wa vijiji vya Wangutwa na Igelango kuonesha ushirikiano wa kulinda na kuwakamata wanaotoaalama  za kuweka nguzo za umeme   huo  Ambapo  viongozi na wadau wengine wanatakiwa kuelimisha wananchi ili wasiriki kulinda miundo mbinu hoyo.

Akizungumza na  Meneja wa Kanda ya nyanda za juu kusini magharibi anayesimamia utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijiji REA Kwa mikoa ya Katavi,Mbeya,Rukwa ,Iringa na Njombe Bi.Salome Mkondora  amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia hamsini na kwamba mwanzoni mwa mwezi Decemba wanategemea kuwa wamewasha upande wa Ilembula.

Kwa Upande wao wananchi wa Vijiji vya Igelango kata za Uhambule na Ilembula wamekanusha kuharimu miundombinu ya umeme iliyowekwa na wakandarasi kwaajili ya kufikisha mradi huo na kwamba wanaahidi kushirikiana na viongozi wao kuimalisha ulizi wa miundombinu hiyo Ambapo wameseam kama kuna mtu anaharibu huenda wakawa ni watoto.

No comments:

Post a Comment