Tuesday, October 21, 2014
BASI LA MWAFRIKA LA SABABISHA MAJERUHI 32 ASUBUHI YA LEO
KAMANDA WA POLISI MKOA WA NJOMBE SACP FULGENCE NGONYANI AKIWA OFISINI KWAKE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
Jumla ya Majeruhi 32 wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe ya Kibena Wakipatiwa matibabu kufuatia kutokea kwa ajali ya gari la Kampuni ya Mwafrika iliyotekea leo majira ya saa nne asubuhi wakati basi hilo likitokea Wilayani Makete kuelekea Mkoani Iringa.
Wakizungumza na Uplands fm Baadhi ya Majeruhi wa Ajali hiyo wamesema kuwa Aajali hiyo imetokana na Mwendokasi wa dereva wa gari hilo Ambapo wamesema alijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake Jambo ambalo limesababisha kuacha njia na kuingia kwenye mtaro wa maji na kusababisha majeruhi hao.
Aidha Majeruhi hao wamesema basi hilo lilikuwa likitokea Wilayani Makete likielekea Mkoani Iringa limesababisha Majeruhi Mbalimbali Wakiwemo walikuwa wakitokea katika Hospitali ya Ikonda baada ya kupata unafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani na kukutwa na ajali hiyo.
Akizungumza na Uplands fm Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kibena Dr Patrick Msigwa Amesema kuanzia majira ya saa nne na nusu wameanza kupokea majeruhi Ambao wamefikia idadi ya watu 32 waliojeruhiwa Ambapo hadi sasa majeruhi watatu wameruhusiwa kwenda katika hospitali ya Ikonda kuendelea na matibabu.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani amethibitisha kutokea kwa Ajali hiyo na kusema kuwa Gari la Kampuni ya Mwafrika lenye Namba za Usajiri T 726 AGA aina ya Scania liliacha njia na kuanguka na kusababisha majeruhi hao katika eneo la mashamba ya chai Kibena.
Kamanda Ngonyani amesema Majeruhi Watatu wameruhusiwa kwenda Nyumbani Ambapo wengine bado wapo katika Hospitali ya Kibena wakipatiwa Matibabu na kuwataja Majeruhi Wawili waliozidiwa kuwa ni pamoja na Aidan Sekrand 72 Mkazi wa Makete ambaye amevujika mikono yote miwili na Janne Chengula 49 Mkazi wa Makangalawe Wilayani Makete aliyevunjika mkono mmoja mara tatu.
Kufuatia Kutokea kwa ajali zinazosababishwa na Uzembe wa Madereva wa Vyombo vya Moto Kamanda Ngonyani ametumia Fursa hiyo kuwataka madereva wote kutii sheria bila shuruti kwa kupunguza Mwendokasi wakiwa barabarani ili kupunguza Ajali zisizo za lazima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment