Waziri wa malisiali na utalii Lazaro
Nyalandu (mwenye suti wa tano kushoto ) akiwa katika picha ya pamoja na
maaskofu wa kanisa la Anglikana Tanzania na mbunge wa jimbo la Ludewa
Deo Filikunjombe mwenye suti wa tatu kushoto ,askofu mkuu wa
Anglikana Tanzania Jacob Chimeledya ,askofu mpya wa Dayosisi ya
Tanganyika kusini Magharib Methew Mhagama na wa kwanza kulia mkuu wa
wilaya ya Njombe Sarah Dumba
WAKATI
hadi hivi sasa makundi ya wagombea Urais yakiendelea kukitesa
chama cha mapinduzi (CCM) kutokana na idadi ndefu ya wanachama
wanaotaka nafasi ya kuingia Ikulu baada ya Rais Jakaya Kikwete
,askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika kusini
Magharibi Mathew Wilfred Mhagama ameibuka na kusema kuwa ili
kuliunganisha Taifa la Tanzania kuwa moja ni vema Rais ajaye mwaka
2015 atoke Zanzibar na si vinginevyo.
"
Ninawaomba sana wakristo wa dayosisi hii na kote Tanzania Rais
ajaye ataongozwa na katiba na sio dini yake hivyo nawaomba sana
tuheshimu mapatano yetu ..... tuombe vyama vya siasa visome
alama za nyakati kwa kutumia vema maamuzi ambayo yataliunganisha
Taifa hili"
Askofu
huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Njombe mara baada ya
kusimikwa kuwa askofu mpya wa nane wa Dayosisi hiyo baada ya
askofu aliyekuwepo kufariki duni ,sherehe iliyohudhuriwa na waziri
mkuu Mizengo Pinda kwa kuwakilishwa na waziri wa maliasili na utalii
Bw Lazaro Nyalandu.
Alisema
kuwa wito wake kwa viongozi wa umma wanapokubali kupongezwa pia
wawe tayari kukosolewa badala ya
kutangulia kiburi pale wanapokosolewa hivyo alisema ni heri kanisa
kutimiza wajibu wake kama mtume wa Mungu kuliko kunyamaza kimya .
Askofu
Mhagama alisema kuwa Taifa letu limekuwa likipita katika
mabadiliko hivyo lazima waumini wa madhehebu yote kuendelea
kumwomba Mungu ili kufanikisha kuvuka salama katika mabadiliko
makubwa ambayo nchi inakwenda nayo kwa sasa .
"
Ni Lazima kumwomba sana Mungu ili atusaidie kutuvusha salama
ilazima tuombe bila kukoma pia nashukuru tume ya Jaji Wariomba
kwa kazi yake nzuri ya kukusanya maoni ya watanzania katika
mchakato wa katiba mpya uliomalizika hivi karibuni mjini
Dodoma...... Zanzibar inahitaji kuzaliwa kwa mara ya pili ili
kuepuka na siasa na watu kusahau yaliyopita kwa kuwa na zanzibar
mpya
ya watu yenye kuaminiana na kuvumiliana kwani Tanzania bila
Zanzibar haipo .....uchaguzi uliopita nilipiga kura katika jimbo
langu la Mkunazini Zanzibar na kura ya Urais nilimpigia Dr Ally
Mohamed Shein wa CCM na kura ya uwakilishi nilimpigia Juma Jusa (
CUF) japo kuna wakati alinikwaza sana kutokana na kauli zake
...sikupigia chama nilipigia umoja na watu timamu hivyo hekima za
Suleiman zinahitajika ili kulifanya Taifa hili kuwa mmoja hivyo
Rais wetu tutakae mchagua atafungwa na katiba ya Jamhuri ya muungano
wa Tanzania na sio dini yake dini itamsaidia yeye kuwa karibu na
Mungu wake ila katiba itatusaidia sisi ambao si wa dini yake hivyo
ni vizuri tukaipa
nafasi hekima ili Rais wa 2015 wa Tanzania atoke Zanzibar ili
isifikie mahali Zanzibar wakaona wanatumika "
Askofu
huyo ambae wazazi wake ni wazaziliwa wa mkoa wa Njombe ambao
walihamia Zanzibar kikazi ambako pia alizaliwa huko na kuendelea
kuifanya kazi ya huduma za kiroho huku kabla ya kuchaguliwa kuwa askofu
wakanisa hilo alisema kuwa moja kati ya mkakati wake akiwa katika
Dayosisi hiyo ni kuona anaanzisha mfuko wa kusaidia
watoto wenye matatizo kielimu na kuwa mfuko huo unahitaji kiasi cha
Tsh milioni 50 ili kuanza na kuwa kamwe hatakubali kuona watu ama
mtu anajinufaisha na mali za dayosisi hiyo ama vinginevyo kwa faida
yake.
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akitoa
salam zake kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Njombe aliwaomba waumini
wa dini hiyo na madhehebu mengine yote kuendelea kuliombea
Taifa ili lidumu katika amani ,upendo na mshikamano .
Filikunjombe
alisema kuwa jukumu la kuendelea kuliombea Taifa hili ni jukumu
la kila mtanzania hivyo alisema kuwa kama ilivyokuwa katika
uchaguzi wa askofu huyo ulifanywa na waumini wake ila bado maombi
ya waumini wa dini zote yalitawala katika kanisa hilo na ndio
maana uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na upendo zaidi .
Pia
mbunge huyo alipongeza kazi nzuri zinazofanywa na kanisa hilo
katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Dodosisi hiyo wakiwemo
wananchi wa jimbo lake la Ludewa hasa katika kijiji cha Mbongo
ambako kanisa hilo limejitolea kujenga Zahanati na kuwa huduma
hiyo inasaidia watu wote bila kuangalia dini wala vyama vyao.
"
Niseme machache kwa niaba ya wananchi wa Ludewa wanakuombea kwa
mwenyezi Mungu vitu vitatu ,kwanza kuwa na afya njema na uzima , pili
uwe na uvumilivu na zawadi ya tatu kuendelea kuwa na busara
zaidi....mwisho niseme mimi ni kiongozi wa mhilimi mwingine kuna
serikali ,mahakama na bunge naomba sana maaskofu na viongo\zi wote wa
dini mtuombee ili mwenyezi Mungu aguse mioyo yetu na tuweze kutenda
yale ambayo yana saidia kuwakomboa watanzania wote"
Akitoa
salam zake kwa niaba ya waziri mkuu Pinda ,waziri Nyalandu alisema
kuwa serikali ni sikivu na imesikiliza yote ambayo yanazungumzwa
na wananchi wake na kuwa katiba zote zitaendelea kuheshimu Uhuru
wa kuabudu .
Kwani
alisema kuwa mbali ya taifa la Tanzania kuendelea kukua kwa kasi
ila zipo changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikilikabili
taifa hasa katika kundi la vijana ambao wameendelea kudai
kusaidia changamoto mbali mbali na kuwa serikali itafanya kazi ya
kuwaenzi vijana hata kama wamekengeuka kwa kuwarejesha katika
mstari hasa ukizingatia kuwa vijana ni kiini cha Taifa na wakati huu
ni wakati wa Tanzania yenye mafanikio kuwadia.
MWISHO |
No comments:
Post a Comment