WANAFUNZI WA AGNESS TRUST WAKIONESHA BURUDANI MBELE YA WAGENI RASMI
MKURUGENZI WA AGNESS TRUST AITOA NASAHA
Jumla Ya Wanafunzi 34 Wanatarajia Kufanya Mtihani Wa Kidato Cha Nne Katika Shule Ya Sekondari Agnes Trust Ambapo Pamoja Na Mambo Mengine Wanafunzi Hao Wametakiwa Kwenda Kuwasaidia Wazazi Kufanya Kazi Za Mikono Na Kuepukana Na Tabia Ya Kuzurula Na Kushinda Vijiweni Wakati Wakijiandaa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Kwa Watakaofaulu.
Rai Hiyo Imetolewa Na Katibu Msaidizi Wa Tahosa Ambaye Ni Mkuu Wa Shule Ya Sekondari Mpechi Bwana Peter Mwavela Wakati Akiwa Mgeni Rasmi Katika Mahafari Ya Pili Ya Kidato Cha Nne Ya Shule Ya Sekondari Agnes Trust Ambapo Amesema Wazazi Wanatakiwa Kwenda Kuwaendeleza Na Masomo Ya Ziada Wakati Wakisubiri Matokeo Ili Wanafunzi Hao Wasipate Muda Wa Kuzurula Mitaani.
Bwana Mwavela Amesema Kuwa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Ina Jumla Ya Shule 27 Ambapo Shule Ya Sekondari Agnes Trust Imekuwa Miongoni Mwa Shule Zinazofaulisha
Vizuri Na Kuwaomba Walimu Wa Shule Hiyo Kuendelea Na Jitihada Za Kuwalea Na
Kufundisha Watoto Katika Misingi Ya Maadili Ya Kidini,Kielimu Na Ujasiliamali Ambao
Umekuwa Ukifundishwa Kwa Wanafunzi Wa Shule Hiyo.
Aidha Bwana Mwavela Amekemea Tabia Ya Vijana Kujihusisha Na Matukio Ya Wizi Na
Ukiukaji Wa Maadili Kwa Kuvaa Mavazi Yasiyo Stahili Kwa Jamii Tofauti Na Waliofundishwa Wakiwa Shuleni Na Kusema Kuwa Wanatakiwa Kusoma Kwa Malengo Huku Wazazi Wakiwalea Kwa Maadili Mema Na Kukemea Tabia Mbaya Zitakazofanywa Na Wanafunzi Hao Watakapo Kuwa Nyumbani.
Kwa Upande Wake Mkurugenzi Wa Shule Ya Sekondari Agnes Trust Bi.Agnes Temu
Amewataka Wanafunzi Kwenda Kujishughulisha Nyumbani Kwa Kufanya Kazi Kwani
Amewafundisha Shughuli Mbalimbali Za Kijasilimali Na Kuwaheshimu Walezi Na Wazazi Na Kusema Kuwa Kwa Wale Yatima Hawatakiwi Wanatakiwa Kuzitumia Mbinu Walizofundishwa Shuleni Hapo Na Namna Ya Kuishi Na Walezi Na Wazazi Kwa Kufanya Kazi Kwa Juhudi Na Kutii Maagizo Ya Walezi Na Wazazi Wao.
Amesema Wahitimu Wanatakiwa Kujenga Tabia Njema Kwa Jamii , Kuwa Wabunifu Na
Kwamba Watoto Wengi Wamekuwa Wakisingizia Kuwa Ni Yatima Jambo Ambalo Mkurugenzi Huyo Amepingana Na Mawazo Hayo Kwa Kusema Wanafunzi Wengi Wakitoka Shuleni Huanza Kuendekeza Uzembe Nyumbani Kutokana Na Baadhi Ya Wazazi Kutowafutilia Jambo Ambalo Baadhi Yao Wanaingia Kwenye Matukio Ya Wizi Na Matumizi Ya Madawa Ya Kulevya.
Akisoma Risala Kwa Niaba Ya Wanafunzi Wanaohitimu Elimu Ya Kidato Cha Nne Anitha
Boniface Mayugi Amewashukuru Walimu Kwa Kuwafundisha Taaluma Na Maadili Shuleni
Na Kwamba Wanaomba Wastani Wa 45 Uongezwe Na Kufikia Wastani Wa Asilimia 55 Ili
Kupata Wanafunzi Wenye Ufaulu Wa Juu Katika Mitihani Ya Kitaifa.
No comments:
Post a Comment