ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA SHIRIKA LA HEIFER INTERNATIONAL STEVE DENNE NCHINI
Mfugaji wa Heifer International Tanzania Abel Mwakatumbula na mkewe wakiwa na Makamu wa Rais wa shirika hilo.
Makamu
wa Rais wa Heifer International Steve Denne, Mkurugenzi wa Heifer
International Tanzania Dk. Henry Njakoi wakifurahia mafanikio ya miradi
ya Heifer International.
Makamu wa Rais wa Heifer International akigawa mtamba kwa mwana kikundi cha Faraja Wilayani Rungwe.
Steve Denne akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Abbas Kandoro alipotembelea ofisi za Mkoa.
Steve
Denne alitembelea Tanzania kwa mara kwanza wiki iliyopita kuona miradi
inayoendeshwa na shirika hilo. Katika ziara hiyo, Steve Denne
alitembelea ofisi za mkoa wa Mbeya akifuatana na Mkurugenzi wa Heifer
International Tanzania Dk Henry Njakoi, Meneja Mradi wa EADD Tanzania
Bwana Mark Tsoxo, ambapo walikutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro.
Katika
Mazungumzo yake na Mheshimiwa Abbas Kandoro, Bw Denne aliishukuru sana
serekali ya Tanzania kwa mahusiano mazuri na ushirikiano mkubwa kwenye
kutekeleza miradi ya shirika hilo nchini na hasa katika kuanzisha Mradi
wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD).
Aliahidi
kuwa shirika hilo kupitia mradi wa EADD na miradi mingine tarajiwa,
litaendelea kuleta mabadiliko kwa kuwasaidia wafugaji wadogo kwenye
mikoa wa Mbeya, Iringa na Njombe ili kuinua uchumi wao na kuwa na
ufugaji wenye tija na endelevu.
Pamoja
na miradi aliyoitembelea Steve Denne, mradi wa Uendelezaji Sekta ya
Maziwa Afrika Mashariki (EADD) unaoanza Mkoani Mbeya wilaya ya Rungwe
kijiji cha Kyimo ambapo aligawa mtamba kwa mfugaji wa kikundi cha Faraja
kama dira ya shirika hilo ya “Toa Zawadi Pia” – Pass On The Gift.
Akiwa
nchini, Makamu wa Rais wa shirika la Heifer International alikutana na
wadau mbalimbali wa sekta ya maziwa nchini wakiwemo wasindikaji, Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Zanzibar ambapo alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Kassim
Gharib Juma.
Makamu
wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne, Meneja Mradi wa
EADD Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika picha ya
pamoja.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana akiwakaribisha ofisini
kwake, Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne na
Mkurugenzi wa Shirika hilo Tanzania Dk. Henry Njakoi.
Steve Denne alipomtembelea Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana.
Steve Denne katika mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dk. Kassim Gharib Juma
(kushoto) akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer
International Steve Denne na Dk. Henry Njakoi, Mkurugenzi wa Shirika
hilo nchini.
No comments:
Post a Comment