WAHITIMU WAKIBURUDISHA NA WIMBO WA KWAYA
WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI
HAWA NI WANAFUNZI WAAGWA WA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI ILOVI KATA YA MAKOGA
MGENI RASIMI AMBAYE NI DIWANI WA KATA YA MAKOGA BWANA ABRAHAM CHAULA AKITOA HOTUBA KWA WAZAZI KATIKA MAHAFARI YA 41 YA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA MSINGI ILOVI WILAYANI WANGING'OMBE
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MAKOGA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ILOVI
BAADHI YA WAZAZI WAKISIKILIZA KWA UMAKINI HOTUBA YA MGENI RASMI
Wazazi na Walezi wa kata ya Makoga Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe wametakiwa kutowaruhusu watoto waliohitimu elimu ya darasa la Saba mwaka huu kwenda kufanya kazi za ndani Mijini kama ilivyozoeleka na waliowengi hapa nchini kwamba Mikoa ya Njombe na Iringa ndiyo ya kuchukua wafanyakazi wa ndani.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa kata ya Makoga bwana Abrahamu Chaula wakati akiwa Mgeni rasmi kwenye mahafari ya 41 ya darasa la saba katika shule ya msingi Ilovi Ambapo amesema kwa mzazi yeyote atakayempeleka mtoto aliyemaliza darasa la saba kwa ndugu zake pasipo kibali maalumu toka serikalini Hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Akijibu baadhi ya changamoto zinazoikabili shule ya msingi Ilovi iliyopo kata ya Makoga bwana Chaula amesema kuwa serikali ya kijiji cha Makoga kwa kushirikiana na wadau wa elimu inatakiwa kuanza mipango ya ukarabati wa nyumba za walimu kila mwaka huku wadau wa elimu wakiombwa kusaidia kuchangia ununuzi wa samani za shule huku akiahidi kuzifikisha changamoto nyingine kwa afisa elimu wilaya ya Wanging'ombe.
Omary Mwalongo ni Mwenyekikiti wa kijiji cha Mkoga ambaye amesema amepokea agizo la Diwani wa kata hiyo la kusimamia watoto wasipelekwa kwenye kazi za ndani na kwamba kwa atakayechaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari na wengine wakipelekwa katika masomo ya vyuo vya ufundi stadi.
Akisoma Risala fupi kwa Mgeni rasmi kwa niaba ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ilovi bwana Nehemia Mhepela,muhasibu wa shule hiyo Bi. Anna Mwinuka amesema shule ya msingi Ilovi imefanikiwa kupunguza changamoto ya utoro kwa watoto shuleni kutokana na kutolewa kwa chakula shuleni.
Bi. Mwinuka amesema kuwa Shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa nyumba za walimu,uchakavu wa madarasa pamoja na upungufu wa samani za shule na fedha za kuendeshea.
Shule ya Msingi Ilovi ilianzishwa mwaka 1955 lakini bado inatumia madarasa yalijengwa mwaka huo na Inajumla ya wanafunzi mia tatu tisini na tatu na walioagwa ni wanafunzi 43 Ambapo wazazi wameshukuru kwa jitihada za walimu wa shule hiyo kwa kufundisha maadili na kuboresha taaluma shuleni na hivyo wazazi hao wamelazimika kuwazawadia chupa 10 za chai zenye thamani ya zaidi ya shilingi elfu sabini na nne.
No comments:
Post a Comment