Monday, September 15, 2014
MAJAMBAZI SUGU WATANO WAKAMATWA MKOANI NJOMBE
KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE SACP FULGENCE NGONYANI AKIWA OFISINI KWAKE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
Na Michael Ngilangwa-Njombe..
Watu Watano Wanaosadikiwa Kuwa Ni Majambazi Sugu Wamekamatwa Na Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Wakati Wa Msako Ulioendeshwa Na Jeshi Hilo Kuanzia
September 12 Hadi 14 Mwaka Huu Na Kuwakamata Watuhumiwa Hao Wakiwa Na Mali Mbalimbali Zinazodaiwa Kubwa Mkoani Hapa.
Miongoni Mwa Watuhumiwa Waliokamatwa Katika Msako Huo Ni Pamoja Na Omary Kawogo Mwenye Umri Wa Miaka 25 Mkazi Wa Makambako,Geofrey Mgen Maarufu Kwa Jina La James Mwenye Umri Wa Miaka 29 Mkazi Wa Wilaya Ya Makete,Roscas Sanga Maarufu Kwa Jina La Rodrick Mwalongo Mwenye Umri Wa Miaka 35,Michael Mgimba 20 Mkazi Wa Mtaa Wa Msikitini Njombe Na Oscar Fwalo Mwenye Umri Wa Miaka 18 Mkazi Wa Mtaa Wa Msikiti Wa Njombe Mjini.
Akizungumza Na Uplands Fm Akiwa Ofisini Kwake Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Fulgence Ngonyani Amesema Kufuatia Kukamatwa Kwa Watuhumiwa Hao,Wananchi Wa Mkoa Wa Njombe Wanatakiwa Kufika Katika Ofisi Za Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Ili Kutambua Mali Mbalimbali Walizoibiwa Kwenye Ofisi Na Nyumbani Mwao.
Aidha Kamanda Ngonyani Amesema Jumla Ya Mali 23 Zinazosadikiwa Kuwa Ni Za
Wizi Zimekamatwa Kwa Watuhumiwa Hao Ambapo Baadhi Ya Mali Hizo Ni Pamoja Na Funguo Za Gari Moja Na Pikipiki Aina Ya T BETTER NO. T 720 CTV,Kichwa Cha Cherehani,Camera 350 AF,Spika Kubwa 4 Pamoja Na Radio Saboofer 4,TV Flat 3.
Matukio Ya Wizi Wa Mali Yamekuwa Yakijitokeza Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Njombe Ambapo Wananchi Wamekuwa Wakivunjiwa Nyumba Zao Na Milango Ya Biashara Huku Wengine Wakivamiwa Na Kupolwa Mali Zao Nyakati Za Usiku Na Watu Wanaosadikikiwa Kuwa Ni Majambazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment