Tuesday, September 30, 2014
BARAZA LA WAZEE LAIOMBA SERIKALI KUTUNGA SHERIA YA KUCHANA NGUO ZA KUZALILISHA KWA WADADA NA MILEGEZEO KWA WAKIUME HADHARANI
MWENYEKITI WA WAZEE KATA YA MAKOGA AKIFUNGUA SHEREHE
ISKAKA MSIGWA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA PADI
WAZEE WA KATA YA MAKOGA WAKISIKILIZA KWA UMAKINI
ABRAHAMU CHAULA NI MGENI RASMI AMBAYE PIA NI DIWANI WA KATA YA MAKOGA
Baraza la Wazee wa Kata ya Makoga wameiomba Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe kutunga sheria ndogondogo za kuwaruhusu wananchi kuchana Mavazi ya aibu yanayovaliwa na baadhi ya Vijana wa Kiume na wa kike wakiwemo mabaamedi ili kutunza maadili kwa vijana wengine wasiyo na tabia kama hizo.
Wakizungumza mara baada ya Maadhimisho ya siku ya wazee kata ya Makoga Wazee hao wamesema kumekuwa na baadhi ya vijana wakiume na wa kike kuwa na tabia ya kuvaa milegezeo ya suruali na Wasichana kuvaa suruali za kubana na kuchora maumbile yao na sketi fupi zenye mipasuo hususani mabinti wanaouza pombe kwenye grocari yaani mabaamedi Na kwamba Matendo hayo yanalidharirisha Taifa.
Aidha Wzee hao wameomba serikali za Vijiji,kata na Halmashauri kuwashirikisha kwenye Vikao vya maamuzi,kuwapatia matibabu Bure kama sera ya Taifa Inavyosema kwa vituo vyote vya afya,kuweka mikakati madhubuti ya kudhibiti unyanyasaji wa Kijinsia na Mauaji ya Vikongwe yanayotokana na Imani za Kishirikina pamoja na kuwapatia pesheni za Uzeeni.
Akisoma Taarifa Fupi mbele ya Mgeni Rasmi Muwakilishi wa Baraza la Wazee Wilaya ya Njombe na Kata ya Makoga bwana Daud Mgeyekwa Amesema kuwa baraza la Wazee kata ya Makoga lilianzishwa mwaka 2011 chini ya shirika la PADI Kwa lengo la Kutetea haki za wazee Ambapo limefanikiwa kupata mikopo midogomidogo kupitia shirika la PADI ambayo imesaidia kuendesha miradi ya ufugaji kuku,nguruwe na bustani.
Abrahamu Chaula ni diwani wa Kata ya Mkoga Wilayani Wanging'ombe Akiwa Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho hayo amesema kuwa kuanzia sasa wazee watakuwa wanashiriki kwenye maamuzi ya maendeleo ya kata na kuwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha wanawashirikisha katika kujadili vikao vya ndani pasipo kuwatenga.
Aidha bwana Chaula amesema kuwa kutokana na changamoto zinazowakabili baadhi ya Wazee za kutopatiwa matibabu Bure kwenye zahanati zilizoko kwenye vijiji vya kata hiyo wanatakiwa kutoa taarifa kwa uongozi wa kata ili kumuwajibisha anayeshindwa kuwasaidia wazee kutibiwa bure na kumpeleka kwa Mkurugenzi wake apatiwe adhabu.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema serikali inalo jukumu la kuwatimizia mahitaji wazee pamoja na Jamii kuwajali kwa kutowanyanyapa,kuwanyanyasa na kwamba lengo la kuanzisha shirika hilo ni kuwasaidia wazee kupata huduma mbalimbali ambazo zimekuwa haziwafikii wazee ikiwemo matibabu bure.
Maadhimisho hayo ya Wazee yamefanyikia kijiji cha Uhekule kata ya Makoga Wilayani Wangingombe huku Mbunge wa jimbo la Njombe amagharibi akichangia shilingi laki tatu na mdau wa wazee akichangia shilingi laki moja ambazo zimekabidhiwa kwa wazee na diwani huyo Ambapo leo maadhimisho hayo kimkoa yanataraji kufanyika katika Taarafa ya Igominyi Mkoani Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment