Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, April 24, 2014

MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AAGIZA WAZAZI KUPELEKA WATOTO KUPATIWA CHANJO YA MATONE KWA WATOTO CHINI YA MWAKA MMOJA



MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI MJINI MAKAMBAKO KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA CHANJO

Wazazi Mkoani Njombe Wametakiwa Kuhakikisha Chanjo ya Matone Kwa Watoto

Waliochini Ya Umri wa Mwaka Mmoja Inatolewa Kwa Watoto Hao Kwa Ajili ya Kinga ya

Magonjwa Nyemelezi Pamoja na Magonjwa Ambukizi Ili Kuepusha Vifo Vinavyotokana

Magonjwa Hayo.

Rai Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi,Sarah Dumba Katika Uzinduzi wa

Wiki ya Chanjo Kitaifa Ambapo Kwa Mkoa wa Njombe Yanafanyika Katika Halmashauri ya

Mji Wa Makambako Ambapo Amesema Kuwa Kila Mzazi Anatakiwa Kuhakikisha Mtoto

Anapata Chanjo ya Matone Ili Kutekeleza Sera ya Taifa Pamoja na Kuwakinga Watoto Na

Magonjwa Shambulizi Kwa Watoto Wenye Umri wa Mwaka Mmoja.

Bi,Dumba Amesema Kuwa Sababu za Kufanya Wiki ya Chanjo Kitaifa Ni Kuhamasisha

Watu Woye Nchini Ili Wahakikishe Watoto Wanaostahili Kupata Chanjo Hiyo Wanapatiwa

Ili Kuwakinga Na Magonjwa yanayozuilika Kwa Chanjo,Kama Hapa Anavyosema,

Aidha Katika Risala Iliyosomwa na Afisa Afya Mkoa wa Njombe Bi,Linda Chatila Kwa

Mgeni Rasmi Bi,Dumba Imeleza Changamoto Mbalimbali Inayokabiliwa Nayo Idara ya

Afya Katika Mkoa wa Njombe, Kama Hapa Anavyosoma.

Pamoja na Mambo Mengine Risala Hiyo Imeeleza Mikakati Ambayo Inatarajia  Kufanyika

Katika Idara ya Afya Kuwa ni Pamoja na Kuhakikisha Kila Kituo Kinatoa Huduma ya

Chanjo,Kuwajengea Watoa Huduma Hiyo Uwezo Wa Kutoa Huduma Bora Kwa

Jamii,Kujenga Maabara Bora ya Mkoa Pamoja na Kutoa Elimu Kwa Jamii Namna ya

Kukabiliana Na Magonjwa Yanayoweza Kuzuilika Kwa  Chanjo.

Kwa Upande WakeMratibu wa Uzazi na Mtoto Mkoa wa Njombe Bi,Felisia Hyera Amesea

Kila Mzazi Anatakiwa Kuhakikisha Mtoto Anakamilisha Kupata Chanjo Zote Tano Kabla

Ya Kufikisha Umri wa Mwaka Mmoja Ili Kumkinga Dhidi ya Magonjwa Hayo Yanayoweza

Kuzuilika.

Kauli Mbiu ya Wiki ya Chanjo Kitaifa Inasema"CHANJO NI JUKUMU LETU SOTE"

Ikienda Sambamba Pamoja na  Ujumbe Unaosema"JAMII ILIYOKAMILISHA CHANJO

NI JAMII YENYE AFYA BORA"

No comments:

Post a Comment