Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, November 16, 2013

UKARABATI WA MUDA WA BARABARA KATIKA KATA YA MJIMWEMA WATARAJIA KUANZA MWAKA HUU MJINI NJOMBE



 DIWANI WA KATA YA MJIMWEMA JIMMY NGUMBUKE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI AKIWA KATIKA OFISI YA MTAA WA JOSHONI KUHUSIANA NA MAREKEBISHO YA BAADHI YA BARABARA
 KWA MUJIBU WA MAELEZO YA DIWANI BARABARA HII FEDHA BADO HAZIJATOKA KWAAJILI YA KUTENGENEZEA MITARO YA MAJI HIVYO HUENDA ISITENGENEZWE MWAKA HUU.




HII NI BARABARA AMBAYO WANANCHI WA MITAA HIYO YA MPECHI NA JOSHONI WAMEKUWA WAKILALAMIKIA KWAMBA INAHATARISHA USALAMA WA WATOTO NA WATU WAZIMA MSIMU WA MVUA KUTOKANA NA MAJI YA MVUA KUTILILIKA KWA WINGI HUENDA YAKAWACHUKUA WATOTO WAKAPOTEZA MAISHA KWA KIFO CHA MAJI.

Serikali Wilayani Njombe Inatarajia Kuanza Kufanya Ukarabati wa Muda wa Barabara za Mitaa ya Mpechi na Joshoni Mjini Njombe Kufuatia Barabara Hizo Kuharibika na Wakati Mwingine Kuhatarisha Maisha ya Wananchi wa Mitaa Hiyo Kutokana na Barabara Hizo Kuchimbika na Kuwa Makorongo.

Diwani wa Kata ya Mjimwema Jimmy Ngumbuke Amesema Katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 Serikali Inatarajia Kufanya Ukarabati wa Barabara Hizo Kwa Kuanza Kuchimba Mitaro na Kufukia Mashimo Katika Mtaa wa Joshoni Eneo la Makaburini na Kumaliza Kero za Wananchi wa Mitaa Hiyo Inayowakabili Kwa Muda Mrefu.

Akielezea Sababu za Kuchelewa Kuanza Kwa Ukarabati wa Barabara za Mitaa Hiyo Diwani Ngumbuke Amesema Inatokana na Kuchelewa Kwa Fedha Kutoka Mfuko wa Barabara Taifa Kwa Ajili ya Matengenezo ya Barabara na  Kwamba Kwasasa Wamepata Fedha Kiasi Kwa Ajili ya Ukarabati wa Miundombinu ya Barabara Ambazo Zitatumika Kwa Baadhi ya Maeneno.

Aidha Diwani Ngumbuke Ameongeza Kuwa Wanatarajia Kuanza Mazungumzo na Mkandarasi Ambaye Ataweza Kufanya Kazi ya Ukarabati Katika Msimu wa Mvua na Kwamba Ukarabati Huo Unatarajiwa Kukamilika Ndani ya Mwaka Huu.

Kwa Muda Mrefu Wakazi wa Mitaa ya Mpechi na Joshoni WamekuwaWakilalamikia Ubovu wa Barabara za Maeneo Yao Hali Ambayo Ina Hatarisha Maisha ya Wakazi Hao Kufuatia Mitaro ya Barabara Hizo Kuchimbika na Kuwa Makorongo.

No comments:

Post a Comment