HAPA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO SOPHIA SIMBA AKITOA HOTUBA YAKE KWA WANANCHI WA KATA YA SAJA
HAPA NI SAJA WAZEE NA VIJANA MBALIMBALI WAPO MAKINI KUMSIKILIZA WAZIRI WAO
WATOTO NAO HAWAKUKAA MBALI KUMSIKILIZA WAZIRI HUYO
SAFU ZA VIONGOZI MBALIMBALI WA UWT NA WATUMISHI WENGINE WA SERIKALI WAKIJIANDAA KUMPOKEA WAZIRI KABLA YA KUWASIRI KWENYE UWANJA WA MKUTANO
WANANCHI WA KATA YA SAJA WAKIHOJI MASWALI MBALIMBALI KWA WAZIRI SIMBA HAPO JANA AKIWA KATIKA KATA HIYO
WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE, JINSIA NA WATOTO
Wananchi wa kata ya Saja Wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe wameiomba serikali
kuwasaidia kusogeza huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo kituo cha polisi, huduma za
afya na maji ambapo pamoja na mambo mengine pia wameomba serikali kusaidia kundi
la walemavu ambalo limedaiwa kuishi maisha ya shida huku likikosa kuthaminiwa pindi
linapokwenda kupatiwa huduma za matibabu.
Wakizungumza mbele ya Waziri wa maendeleo ya jamii, wanawake,jinsia na Watoto
bi.Sophia Simba wananchi wa kata wa kata hiyo wamesema kuwa kata hiyo imekuwa
ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji, huduma za kiafya na
miundombinu mibovu ambapo wameelezea umbali uliopo wa kusafiri kufuata huduma za
kiofisi hususani watumishi wa serikali na kuomba kuendelea kupata huduma katika
halmashauri ya Makambako.
Katika hatua nyingine wananchi hao wamelalamikia kuwepo kwa migogoro ya mipaka kwa
muda mrefu mgogoro unaohusisha vijiji vya Itengero na Kipagamo huku wakiiomba
serikali kutatua mgogoro huo haraka ili kuepukana na madhara yanayoweza kusababishwa
na migogoro hiyo,michango ya shule kushindwa kupatiwa ufafanuzi juu ya matumizi yake
pamoja na watoto kupatiwa adhabu kwa kushindwa kutoa michango.
Akijibu maswali ya wananchi wa kata ya Saja Waziri wa maendeleo ya jamii,wanawake,
jinsia na watoto Sophia Simba amesema kuwa kuhusu kundi la watu wenye ulemavu
halmashauri za wilaya zinatakiwa kuwahudumia kwa kuwatambua kupitia maafisa
maendeleo ya jamii huku akiwataka wananchi kutowaficha watoto wenye ulemavu pamoja
na kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi ikiwemo kituo cha polisi ili kurahisisha
huduma za kijamii.
Aidha bi Simba amewataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho
serikali inajipanga kusogeza huduma mbalimbali za kijamii katika Wilaya ya
Wanging'ombe huku akiahidi kumuagiza mkuu wa mkoa wa Njombe wa Njombe Captain
mstaafu Aseri Msangi kwenda kusikiliza mgogoro wa mipaka unaowakabili wakazi wa
eneo hilo.
Ziara ya Waziri Sophia Simba pamoja na viongozi wengine wa mkoa na kitaifa leo
imeendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Njombe ambapo kesho itahitimishwa Kwa
viongozi wa umoja wa wanawake wa ccm Mkoa na Taifa kutembelea Wilaya za Ludewa na
Makete kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment