Friday, October 25, 2013
SASA MGENI RASMI AMEKWISHA KUWASILI KATIKA UKUMBI WA SHULE YA SEKONDARI RUHUJI HIGH SCHOOL AMEPOKELEWA KWA BURUDANI MBALIMBALI
MKUU WA SHULE YA SEKONDARI RUHUJI AKIWAKARIBISHA WAGENI
Wazazi na Walezi Mkoani Njombe Wameshauriwa Kushirikiana na Walimu Katika Kuhakikisha Kiwango cha Elimu Kinakuwa Huku Wakitakiwa Kuachana na Tabia ya Baadhi ya Wazazi Waliyojijengea ya Kuwaachia Walimu Majukumu Yote ya Kielemu ya Watoto Wao.
Aidha Wazazi na Walezi Hao Wametakiwa Pia Kufuatilia Maendeleo ya Elimu Pamoja na Tabia za Watoto Wao Pindi Wanapotoka Shuleni Kwani Baadhi ya Wanafunzi Hawahudhurii Shuleni na Matokeo Yake Hulaumiwa Walimu.
Kauli Hiyo Imetolewa Wakati wa Mahafari ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Ruhuji na Afisa Elimu Taaluma Shule za Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Zegeli Shengeli Ambapo Amewataka Wanafunzi Hao Kujiepusha na Vitendo Viovu.
Akitolea Ufafanuzi wa Baadhi ya Changamoto Zilizobainishwa Kwenye Risala ya Wahitimu Mkurugenzi wa Shule Hiyo Gordon Ngilangwa Amesema Uongozi wa Shule Sekondari Ruhuji Umeanza Kuweka Mikakati ya Kutatua Changamoto Zinazoikabili Shule Hiyo Ikiwemo Huduma ya Maji Kwa Kuweka Pampu za Hydram.
Awali Wakisoma Risala Kwa Mgeni Rasmi Wahitimu wa Kidato cha Nne Mwaka 2013 Wamebainisha Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Ukosefu wa Nyumba za Walimu Pamoja na Huduma ya Maji Ambapo Pia Wameelezea Baadhi ya Mafanikio ya Shule Hiyo.
Jumla ya Wahitimu Themanini Wanaotarajiwa Kufanya Mitihani ya Mwisho Mwaka Huu Wametunukia Vyeti Vya Kuhitimu Kidato cha Nne.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment