KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN-IRINGA
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa mwenge wa Uhuru unahimiza mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kudumisha amani miongoni mwa watanzania.
Akielezea juu ya maadhimisho hayo alisema kuwa kwa upande wa maadhimisho ya wiki ya vijana ,kuwa maadhimisho hayo yataanza leo na siku ya tarehe 14 kutakuwa na ibada ya kumwombea baba wa taifa na siku hiyo pia mwenge utazimwa.
Hata hivyo alisema kuwa maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na kuwa shughuli mbali mbali za vijana kutoka mikoa mbali mbali Tanzania wanashiriki katika maadhimisho hayo na kuwa vikundi zaidi ya 100 vinaendelea na kuonyesha shughuli za kazi zao.
Pia alisema mbali ya vijana hao kuonyesha kazi zao pia watakuwa na midahalo yao katika ukumbi wa VETA mdahalo utakaoanza kesho jumatano .
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa maadhimisho hayo yanatarajia kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka nchi mbali mbali.
Hivyo kuwataka wakazi wa Iringa kuonyesha uzalendo zaidi kwa wageni watakaofika mkoani hapa .
Kuhusu ulinzi na usalama alisema kuwa serikali imejipanga vema katika kuhakikisha amani inakuwepo na kuwa kwa sasa vitendo vyovyote za uvunjifu wa amani havitavumiliwa na kuwa atakayejihusisha na uvurugaji wa amani atawajibishwa.
Hivyo kuwataka wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa haraka iwapo watakuwepo watu wanaotaka kuvuruga amani.
Napenda kuwapongeza Manispaa ya Iringa kwa kufanya vema katika usafi wa mazingira japo yapo maeneo ambayo bado ni machafu hivyo kila mwananchi kufanya usafi katika maeneo yake.
No comments:
Post a Comment