Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, October 11, 2013

KAMATI YA USHAURI YA WILAYA YA NJOMBE DCC LEO YATEMBELEA NA KUSIKILIZA MATATIZO YANAYOWAKABILI AKINA MAMA NA WATOTO KATIKA TAARAFA YA LUPEMBE





 AFISA TAAFARA YA LUPEMBE BARTAZARY MVEYANGE AKIWAKARIBISHA WAGENI


 WATAALAMU WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE WAKIWA NA WAKAZI WA KATA YA MFRIGA LEO KATIKA SHULE YA MSINGI MFRIGA

 WAJUMBE WA KAMATI YA USHAURI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE WAKIWA NA MWENYEKITI WAO WA KAMATI HIYO AMBAE PIA NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI. SARAH DUMBA













 HOJA YA CHAI IKAWA NI KERO KWA WAKULIMA WA LUPEMBE KWA KUCHUKULIWA WAKATI WA USIKU NA KUWATUMIKISHA WATOTO WA SHULE KUCHUMA CHAI HIYO

 NI MTOTO YATIMA WAJUMBE NA WANANCHI WA KATA YA MFRIGA WAMEMCHANGIA SHILINGI LAKI MOJA NA SITINI KAMA HARAMBEE YA PAPOHAPO KWAAJILI YA MAHITIJI YA SHULE NA NYUMBANI
 NI KWELI MTOTO HUYU ANASTAHILI KUSAIDIWA NI MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MFRINGA WA DARASA LA SITA NGUO NA VIATU KWAKE NI SHIDA
 HUYU NDIE MLEZI WAKE AMBAE AMETEULIWA KUHAKIKISHA FEDHA ZILIZOCHANGWA ZINATUMIKA KWA MAHITAJI YA MTOTO HUYO YA SHULE


HAYA NI NI MIONGONI MWA MAJENG YA MSINGI MFRIGA KATA YA MFRIGA




                                                            
                                                        

HUYU NI MBWA AMBAE WAKAZI WA KATA YA MFRIGA WANAMJALI SANA KWAAJILI YA ULINZI WA MAZAO YAO YASIHARIBIWE NA WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO KAMA NGEDELE
............

Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Njombe DCC Imewataka Wananchi wa Kata ya Idamba Kuondokana na Imani Potofu za Kishirikina Kuhusiana na Matukio ya Kuanguka Kwa Wanafunzi wa Jinsi ya Kike Katika Shule ya Msingi Iwafi.

Akizungumza na Wananchi Kwenye Mkutano wa Hadhara wa Kata ya Idamba Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Dkt. Conrad Ugonile Amesema Tatizo Hilo Linatokana na Mabadiliko ya Mwili Hasa Wale Wanaokaribia Kupevuka.

Nae Mwenyekiti wa Kamati Hiyo ya DDC ambae ni mkuu wa Wilaya ya Njombe  Bi. Sara Dumba Amewashauri Wazazi na Walezi wa Wanafunzi Hao Kujijengea Tabia ya Kuwapima Afya Watoto Wao Ili Kubaini Matatizo Yanayowakabili Huku Akiwataka Viongozi wa Vijiji na Kata Kuwashawishi Wananchi Kutojihusisha na Masuala ya Ushirikina Kwani Yanaweza Kupelekea Kuvunjika Kwa Amani.


Amesema ni vema wananchi wakaondoa shaka badala yake wakawajengea imani ya kujiamini watoto wao pasipo kutoa maneno ya hofu kwa watoto kwa kuwapeleka kwa wanganga wa jadi wakidhani watalimaliza tatizo hilo na kwamba matatizo hayo ni ya kawaida kwa watoto wa kike wanapoelekea kupevuka ndiyo maana huwa yanawakuta wanawake na siyo wakiume.


Awali Wakizungumza Mbele ya Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Njombe Wananchi wa Kata ya Idamba Waliiomba Serikali Kusaidia Kutatua Tatizo Linalowakabili Wanafunzi wa Shule ya Msingi Iwafi  la Kuanguka na Kuweweseka Tatizo Ambalo Lililodumu Takribani Kwa Takribani Muda wa Miezi Minne Hadi Sasa.

Wanafunzi Wanaokabiliwa na Tatizo la Kuanguka na Kuweweseka ni wa Darasa la Tano Hadi la Saba ikiwa ni takribani miezi minne tangu tatizo hilo litokee katika shule ya msingi Iwafi kata ya Idamba wilayani Njombe.


No comments:

Post a Comment