Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, September 8, 2013

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MTITU WILAYA YA KILOLO WAPEWA ELIMU YA MAZINGIRA !

KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN


baadhi ya wanafunzi wakiangalia kwa umakini jinsi ya kutayarisha kiriba kwa ajiri ya kupanda mti au mbegu na anayewalekeza ni Wilngton kinyonge ambaye alionekana kuvutiwa na elimu iliyokuwa inatolewa
wanafunzi wakifanya kwa vitendo kuweka udogo kwenye viriba
 (picha na kayanda mc)

Katika kuhakikisha elimu juu ya mazingira inamfikia kila mwananchi shirika lisilo la kiserikali linalojihususha na utunzaji wa mazingira IRINGA ENVIRONMENTAL PROTECTORS likishirikiana na TREES FOR THE FUTURE kutoka Marekani wameanzisha mpango wa kutoa elimu ya mazingira bure katika shule za msingi na sekondari mkoani Iringa,akiongea na mtandao huu mkurugenzi wa Iringa environmental protectos(I.E.P) amesema kuwa tumeamua kufanya hivyo ili tuweze kuwakuza watoto wetu katika misingi ya kupenda kutunza mazingira na pia tukaona si vema tukazungukia shule za mjini tu,na hivyo tukamua tuzungukie pia vijijini ambako kwa sasa ndiko ambako hari ya uharibifu wa mazingira inazidi kwa kasi ya ajabu hivyo tumeanza na Wilaya ya kilolo kwa awamu ya kwanza na tunategemea itakapo fika mwezi wa kumi tutangeza kasi zaidi na kuzungukia shule karibu zote wilaya ya kilolo,hata hivyo tunaomba mashirika au kampuni yoyote zijitokeze kushirikiana nasi katika kutokomeza uharibifu wa mazingira,alimaliza kusema hayo Bw;Mponzi.
 Aidha mwalimu mkuu wa shule hiyo Erasto Lwiwa ameshukuru shilika hilo kwa kutoa elimu hiyo ambayo wanafunzi wengi wameonekana kufurahia kutokana na kushiriki kwa vitendo kujishughulisha.

No comments:

Post a Comment