Saturday, September 21, 2013
CHUO CHA UUGUZI NA UGANGA WA MENO BULONGWA WILAYANI MAKETE CHA PONGEZWA NA NAIBU WAZIRI WA MAJI
WANACHUO WAKIWA NADINI YA SALE SIKU YA MAHAFARI YAO
MAKAMU ASKOFU WA KANISA LA KILUTHEL WILAYA YA MAKETE
WAZAZI WALIOHUDHULIA MAHAFALI HIYO
WASANII CHIPUKIZI WA MUZIKI WA BONGOFRAVER EMPOWERING WAKITUMBUIZA KATIKA UKUMBI WA CHUO KWENYE MAHAFALI HAYO
MUUGUZI MKUU WA CHUO CHA UUGUZI BULONGWA AKIWARISHA KIAPO WAHITIMU
NAIBU WAZIRI WA MAJI BINILITH MAHENGE AKITOA HOTUBA KATIKA TAASISI YA SAYANSI YA AFYA BULONGWA
OMEGA MWANAFUNZI WA CHUO CHA UGANGA WA MENO AMBAE AMEHITIMU AKIPOKEA CHETI
NAIBU WAZIRI BINILITH MAHENGE AKISALIMIANA NA BAADHI YA WAZAZI AKIWA NJE YA UKUMBI WA TAASISI YA SAYANSI YA AFYA BULONGWA
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA MBUNGE WA MAKETE BINILITH MAHENGE AKIONDOKA BAADA YA KUHITIMISHWA KWA SHEREHE
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Makete Dokta Binilith Mahenge Amewataka Wauguzi na Wataalam wa Afya Kuzingatia Maadili na Kufanya Kazi Kwa Upendo Pamoja na Kutoa Huduma Bora Kwa Wagonjwa Ili Kuhakikisha Kada ya Uuguzi Inaendelea Kujijengea Heshima Kwa Jamii.
Aidha Dokta Mahenge Amewataka Wauguzi Kutumia Muda Wao Kwa Kutoa Huduma Kwa Wananchi na Wagonjwa Badala ya Kutumia Muda Wao Mwingi Kwaajili ya Kazi Mbalimbali Zisizo na Tija Katika Utoaji Huduma Kwa Wananchi.
Akizungumza Wakati wa Mahafali ya Tatu Kwa Wauguzi na Mahafali ya Sita Kwa Waganga wa Meno wa Taasisi ya Sayansi na Afya Bulongwa Wilayani Makete,Naibu Waziri Mahenge Pamoja na Mambo Mengi Amepongeza Hatua za Taasisi Hiyo Kutoa Elimu Ambayo Imesaidia Kutoa Wataalamu Watakaosaidia Kupunguza Tatizo la Wataalam wa Afya Hapa Nchini.
Awali Akisoma Taarifa Fupi ya Taasisi Hiyo,Mkuu wa Chuo Hicho Tekeleza Mahenge Amesema Jumla ya Wahitimu 95 wa Mafunzo ya Uuguzi na Uganga wa Meno Wamehitimu Mafunzo Hayo na Kufanya Idadi ya Wahitimu wa Fani Hizo Kuongezeka Chuoni Hapo Tangu Chuo Hicho Kilipoanzishwa Mwaka 2004.
Kwa Upande Wao Wahitimu wa Mafunzo Hayo Wamesema Watahakikisha Wanatumia Vizuri Taaluma Yao Kwa Kuboresha Huduma za Afya kwa Wananchi na Usimamizi Bora Katika Vituo Vya Afya,Hospitali na Zahanati Zinazotoa Huduma za Afya Hapa Nchini.
Zaidi ya shilingi milioni nne na laki sita zimepatikana katika harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni na madarasa ya taasisi ya sayansi ya afya Bulongwa ambapo pamoja na mambo mengine wananchi mkoani Njombe wametakiwa kuzitumia fursa zilizopo vyuo kikiwemo chuo cha uuguzi na uganga wa meno Bulongwa ili kupiga vita maadui watatu ujinga,maradhi na umasikini.
Akizungumza na wahitimu wa chuo cha uuguzi na uganga wa meno katika taasisi ya sayansi ya afya Bulongwa mwishoni mwa wiki iliyopita Naibu waziri wa maji na Mbunge wa wilaya ya Makete Binilith Mahenge amesema kuwa wilaya ya Makete ina jumla ya vyuo vinne ambavyo vimekuwa vikitoa fursa kwa wanafunzi mbalimbali kujiunga na masomo ya chuo ikiwemo chuo cha ualimu Tandala,chuo cha VETA makete,chuo cha ualimu Bulongwa pamoja na chuo cha sayansi ya afya Bulongwa na kusema vyuo hivyo vinatoa fursa ya elimu.
Aidha Bwana Mahenge amesema kuwa bara la Afrika limekuwa likikumbwa na maadui watatu ambao ni ujinga,maradhi na umasikini ambapo amesema moja ya mambo yaliyofanya Bara la Afrika kuwa nyuma ni kwamba bara hili lipo nyuma katika suala la Sayansi na Technolojia na kusema kuwa jambo hilo linatakiwa kufanyiwa kazi kwa bidii ili kuhakikisha kunakuwepo na wataalamu wa sayansi na technolojia.
Amesema kuwa ni lazima wananchi wawekeze katika elimu ya sayansi na Technolojia ambapo amesema kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa kutumia uzoefu bila elimu ikiwemo suala la biashara,kilimo na sekta mbalimbali za ujasiliamali ambapo sekta ya elimu ikitiliwa mkazo suala la njaa litatoweka.
Wakizungumza kwenye mahafari hiyo baadhi ya wazazi wamewataka wahitimu kuendelea kuongeza bidii katika kazi watakapokuwa kwenye vituo vya kazi na kuondoa tofauti ambazo zimekuwa zikifanywa na wafanyakazi waliotangulia katika vituo vya afya,zahanati na hospitaloi na kwamba kumekuwa na tabia ya kuwanyanyasa wagonjwa na kudharau pamoja na wizi wa dawa zinazotolewa na serikali jambo linalosababisha wagonjwa kukosa huduma muhimu za afya kinyume na maadili ya kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment