Saturday, August 31, 2013
WANANCHI NJOMBE WAPENDEKEZA UWEPO WA SERIKALI TATU KATIKA KATIBA IJAYO
WAKICHANGIA MAONI MBALIMBALI KWENYE RASIMU YA KATIBA MPYA WAKIWA KATIKA UKUMBI WA SHIRIKA LA COMPASSION
Wananchi na Wajumbe Mbalimbali wa Mabaraza ya Katiba Wilayani Njombe Wamependekeza Kuongezwa kwa Muda wa Kujadili na Kutoa Maoni ya Rasimu ya Katiba Katika Awamu Ijayo Ili Kuwa na Uhakika wa Kuijadili Rasimu Hiyo.
Hatua Hiyo Imekuja Wakati Zoezi la Ukusanyaji Maoni ya Undwaji wa Katiba Mpya Kwa Awamu ya Pili Kupitia Mabaraza ya Katiba Ngazi ya Wilaya Likihitimishwa leo Augost 31 Ambapo Wajumbe Mbalimbali Wamepata Fursa ya Kupendekeza Mawazo Yao.
Akizungumza Wakati wa Kuhitimisha Mchakato Huo Katika Shirika la Compasion Foundation Lililopo Mjini Njombe Mwezeshaji wa Mchakato Huo Bwana Andreas Mahali Amesema Kuwa Pamoja na Baadhi ya Wananchi Kushiriki Kikamilifu Katika Zoezi Hilo Lakini Awamu Ijayo ni Bora Muda Ukaongezwa Ili Kuyachambua na Kuyapa Uzito Mambo ya Msingi Katika Katiba.
Aidha Wajumbe Mbalimbali Wametoa Maoni Yao Huku Wengine Wakidai Katiba Mpya Ibainishe Viwanda Kujengwa Mahali Ambapo Malighafi Zinapatikana Huku Wakitaka Wawekezaji Wapewa Muda Maalumu Usioruhusu Kuwekeza Kwa Miaka Mingi.
Katika Hatua Nyingine Wajumbe Hao Wamependekeza Katiba Ijayo Isiwe na Vipengele Vinavyo Ruhusu Kuwepo Kwa Wizara Zisizo Maalumu Ili Kupunguza Bajeti Ya Taifa Isiyo ya Lazima.
Mbali na hayo wananchi hao wamependekeza kuwepo kwa serikali tatu ambapo pamoja na mambo mengine muundo huo utasaidia kupunguza pia gharama na uwajibikaji kikamilifu kwa viongozi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment