Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, August 27, 2013

MGOGORO WA MADINI NJOMBE WAJADILIWA NA MAKAMISHNA WA MADINI KANDA YA KUSINI


MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIWA KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA USALAMA WA TAIFA WILAYA YA NJOMBE NA WAJUMBE WENGINE PAMOJA NA MAKAMISHNA WA NISHATI YA MADINI KANDA YA KUSINI.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba Amewataka Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilayani Njombe Kuzingatia Taratibu za Kuomba Leseni Kwa Wakati Kabla ya Kuanza Shughuli za Uchimbaji Ili Kuhepusha Migogoro Inayotokana na Wachimbaji Wengi Kutozingatia Taratibu Zilizopo Katika Uchimbaji wa Madini.

Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Pia Amewataka Maafisa wa Madini Kuwasaidia Waombaji wa Leseni Kwa Uadilifu na Kwa Kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma Jambo Ambalo Linapaswa Kutekelezwa na Maafisa Hao Ili Kupunguza Migogoro Hiyo.

Akisoma Taarifa ya Mgogoro wa Uchimbaji Madini Katika Kijiji Cha Uliwa Wilayani Njombe,Mbele ya Makamishna wa Madini Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba Amesema Kwasasa Mgogoro Huo Tayari Umeshapatiwa Ufumbuzi Baada ya Pande Zote Kukutanishwa na Kufikia Muafaka Kuhusu Uchimbaji wa Madini Katika Kijiji Hicho.

Amesema Serikali Itaendelea Kusikiliza Kero za Wananchi na Kuhakikisha Inazipatia Ufumbuzi Kadiri Inavyowezekana Huku Akitoa Angalizo Kwa Viongozi wa Vyama Vya Siasa Kuwaeleza Ukweli Wananchi Kuhusu Mambo Yanayojitokeza Katika Maeneo Yao.

Kamishna Msaidizi wa Utoaji wa  lesseni za Madini Kanda ya Kusini John Nayopa Amewataka Watafiti na Waombaji wa Lesseni za Uchimbaji wa Madini Mkoani Njombe Kuhakikisha Wanazingatia Taratibu Zilizopo Ili Kuhepuka Migogoro ya Mara Kwa Mara.

Aidha bwana Nayopa mesema kuwa kwa wachimbaji wadogo wanatakiwa kuzingatia vigezo ambavyo hutolewa na watoa leseni na kwamba katika suala la uchimbaji madini lina ushindani mkubwa hivyo kwa muombaji akikosea kitu kidogo anaweza kukosa nafasi hiyo na ikachukuliwa na nmutu mwingi kulingana na wakati aliokwenda kuomba.

No comments:

Post a Comment