Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, July 12, 2013

WAZIRI MKUU AWAASA WANANCHI KUKINGA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI,AAHIDI KUTENGENEZWA KWA BARABARA ZOTE ZA KUELEKEA WILAYANI KWA MKOA WA NJOMBE










 WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIWASIRI KATIKA UKUMBI WA TURBO MJINI NJOMBE LEO NA KUKAGUA  MIRADI MBALIMBALI  YA WAJASILIAMALI

 MAMA PINDA AKIWAPONGEZA WAJASILIAMALI  KWA JITIHADA WANAZOZIFANYA MKOA WA NJOMBE
 MWENYEKITI WA CCM MKOA WA NJOMBE DEO SANGA AKIZUNGUMZA NA HADHARA KATIKA UKUMBI WA TURBO.
 WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI  WA KUPAMBANA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KILICHOANDALIWA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.
Waziri mkuu Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda leo amemaliza ziara yake na hapa alikuwa katika Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Amezindua Mpango wa Miaka Mitatu wa Kupambana na Maambukizi ya UKIMWI Mkoani Njombe na Kuwataka Wananchi Kubadili Tabia Pamoja na Kuachana na Mila Zinazopelekea Ongezeko la Ugonjwa Huo Mkoani Njombe.

Aidha Waziri Mkuu Pinda Amesisitiza Umuhimu wa Tohara Kwa Wanaume na Kusema Kuwa Hiyo Itasaidia Kupunguza Kiwango Cha Maambukizi Kulingana na Tafiti za Wataalam wa Afya.

Akizungumza Mjini Njombe Wakati wa Uzinduzi wa Mpango Huo Waziri Pinda Amesema Pamoja na Mambo Mengine Mpango Huo Unapaswa Kuenda Sanjari na Badiliko la Tabia Kwa Kila Mtu Kujitokeza na Kupima Afya Yake.

Awali Akielezea Lengo la Mpango Huo,Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Assery Msangi Amesema ni Kwaajili ya Kupanua Kiwango Cha Elimu ya UKIMWI Kwa Wananchi na Kuhakikisha Inatolewa Kwa Kina Huku Kila Halmashauri Ikitakiwa Kutumia Kitabu Hicho Kuelimisha Wananchi.
HABARII HII ITAENDELEA...................HAPA ENDELEA KUTEMBELEA MTANDAO HUU


No comments:

Post a Comment