RPC Mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani akiwa ofisini kwake akizungumza na waandishi wa habari JANA .
Watu Watano Wamefariki Dunia Mkoani Njombe Katika Matukio Tofauti Yakiwemo ya Watu Wawili Waliofariki Kwa Kujinyonga Katika Vijiji Vya Ikang'asi na Mtila Wilayani Njombe.
Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi Fulgency Ngonyani Amewataja Watu Hao Kuwa ni Tucheline Kisakali [65] Mkazi wa Kijiji Cha Ikang'asi Aliefariki Dunia Kwa Kujinyonga Mnamo July 28 Mwaka Huu.
Katika Tukio Jingine Mkazi wa Kijiji Cha Mtila Wilayani Njombe Venance Msemwa [40] Amefariki Dunia Kwa Kujinyonga Kwa Kutumia Kamba ya Katani na Kusema Kuwa Tukio Hilo Limetokea July 28 Mwaka Huu.
Aidha Katika Tukio Jingine Mkazi wa Mbalizi Mkoani Mbeya Eva Mwasakamala [23] Amefariki Akiwa Chumbani Kwake anakolala na Watoto Wake na Kusema Kuwa Mwili wa Marehemu Ulikutwa na Mmoja wa Wakazi wa Kijiji Hicho Ukiwa Chumbani Katika Kijiji Cha Matamba Wilayani Makete.
Katika Hatua Nyingine Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linaendelea na Uchunguzi Juu ya Matukio Kadhaa ya Wizi wa Mali Mbalimbali za Wananchi ukiwemo wizi wa pikipiki.
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limetoa Wito Kwa Wananchi Kutekeleza Kwa Vitendo Dhana ya Utii wa Sheria Bila Shurti
No comments:
Post a Comment