MKURUGENZI WA WIZARA NA MALIASILI NA UTALII VALENTINE MSUSA AKIZUNGUMZA MBELE YA WADAU NA WAKULIMA HAO KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE.
MKURUGENZI WA KIWANDA CHA MIWATI LUSHOTO MKOANI TANGA YUSUPH MULLA
WAKULIMA MBALIMBALI WA KILIMO WAKIWEMO WA CHAI LUPEMBE
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AKIWA NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI SARAH DUMBA WALIOVALIA SUTI NYEUSI MKATIKATI YA MEZA KUU.
Serikali Imewaruhusu Wakulima wa Miti ya Miwati Mkoani Njombe Kufanyabiashara na Wawekezaji Kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Kwa Kuzingatia Sheria na Taratibu za Jumuiya Hiyo.
Kauli Hiyo ya Serikali Imetolewa Leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dokta Lazaro Nyalandu Wakatia Akiongea na Wakulima wa Miti ya Miwati Pamoja na Wawekezaji wa Wanaonunua Maganda ya Miwati Kutoka Viwanda Vya TANWATT Kibena Mjini Njombe na LION WATTLE cha Lushoto Mkoani Tanga.
Aidha Naibu Waziri Nyalandu Amesema Kuwa Kwa Sasa Serikali Itazidi Kulinda Viwanda Vya Ndani Pamoja na Kuwasaidia Wakulima Kukabiliana na Bei Ambazo Haziwanufaishi wa Kulima Zinazotolewa na Wawekezaji Kwa Lengo la Kuinua Kipato cha Wakulima Hapa Nchini.
Awali Wakitoa Malalamikio Yao Mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dokta Nyalandu, Wakulima wa Maganda ya Miti ya Miwati Wamesema Wawekezaji Hao Wamekuwa Wakiwazuia Kuuza Maganda ya Miwati Kwa Wawekezaji Kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Huku Wakiwalipa Fedha Kidogo Zisizolingana na Thamani ya Biashara Hiyo na Kutowalipa Kwa Wakati.
Wakijibu Malalamiko ya Wakulima Hao Mbele ya Naibu Waziri Nyalandu, Mkurugenzi wa Lion Wattle Kilichopo Lushoto Mkoani Tanga Bwana Yusuph Mulla Amesema Hadi Hivi Sasa Hakuna Mkulima Anayekidai Kiwanda Hicho Huku Meneja Misitu wa Kiwanda cha TANWATT Mjini Njombe Bwana Antely Kiwale Akieleza Kuwa Tayari Wamepanga Kukutana na Wakulima Hao Ili Kujadili Gharama za Usafirishaji wa Bidhaa Hizo Kutoka Shambani Hadi Kiwandani Ikiwa ni Pamoja na Kuangali Bei ya Kununulia Bidhaa Hiyo.
No comments:
Post a Comment