Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, June 3, 2013

BAADA YA MWANAWE KUHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KULAWITI, BABA MZAZI APOTEZA FAHAMU MAHAKAMANI.


 Na Ezekiel Kamanga


 Baba Mzazi wa Kijana aliye hukumiwa hukumu ya Miaka 30 Jela, Mzee Mohamedi Nzunja akiwa amepoteza fahamu kufuatia  Hukumu iliyo tolewa kwa Mwanae.

 

 

 Baadhi ya wanafamilia wakifarijiana nje ya Mahakama baada ya ndugu yao kuhukumiwa


 Dada wa Kijana aliye hukumiwa kifungo cha Miaka 30 Jela akiwa ameishiwa nguvu nje ya Mahakama


 Mzee Mohamed Nzunja katikati akinyanyuliwa na mkwewe ili kupelekwa Hospitali .


Mahakama ya wilaya ya Mbeya imemuhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Nsalaga Uyole jijini Mbeya baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wa kidato cha pili jina linahifadhiwa Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Nsalaga.

Mwendesha mashitaka wa Serikali Mheshimiwa Lugano Mwakilasa ameiambia mahakamani hiyo kuwa  Nizra Mohamed (24) mkazi wa Uyole jijini Mbeya alitenda  kosa hilo Novemba 5 mwaka jana (2012) majira ya saa 12 jioni.

Amesema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a 155 sura ya 16 ya marekebisho  kanuni ya adhabu  mwaka 2002 .

Kwa upande Serikali umeleta ushahidi wake ambao ni  Askari walioipeleleza kesi hiyo pamoja na Daktari na binti aliye fanyiwa kitendo hicho

Awali binti huyo ameieleza Mahakamani hiyo kuwa Novemba 5 mwaka jana majira ya saa 12 jioni alivamiwa na mshitakiwa ambaye ni fundi Mwashi Katika eneo la Nsalaga ambapo mshitakiwa  huyo alimkamata kwa nguvu na  kumpeleka ndani ya  nyumba iliyokuwa iaendelea kujengwa (pagara) kisha kumlawiti na kumsababishia maumivu makali hali iliyopelekea kukimbizwa katika hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo Daktari Satumani aliyemfanyia uchunguzi Binti huyo amethibitisha mbele ya mahakama hiyo kuwa binti huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kinyama ambapo alimpa tiba katika hospitali ya Mkoa jijini Mbeya.

Mashahidi wengine  akiwemo  Askari Polisi  amesema kuwa awali mshitakiwa alikili  kosa hilo mbele ya kiapo cha Polisi kituo cha kati Mbeya ambapo mara baada ya uchunguzi kukamilika waliifikisha kesi hiyo mahakamani.

Aidha mshitakiwa huyo alileta mashahidi wawili ambao ni mafundi waashi ambao kwa pamoja walieleza mahakama hiyo kuwa hawa kujua nini kinacho endelea mahakamani hapo.

Baada ya mahakama hiyo chini ya hakimu Gilbert Ndeuruo kuridhishwa na ushahidi kwa pande zote mbili ambapo aliamuru mshitakiwa huyo kutumikia kifungo Cha miaka 30 jela ili iwefundisho kwa wengine.

Pamoja na kupatiwa nafasi ya kujitetea mshitakiwa alishindwa kutoa utetezi wake ambapo ilionekana akijikanyaga mahakamani kwa kusema kuwa hakumbuki kama alimlawiti au kumbaka mwanafunzi huyo hali iliyo mpa fursa Hakimu Ndeuruo kutoa adhabu ya miaka 30 Jela.
 
Hata hivyo ndugu na jamaa wa karibu na mshitakiwa waliangua Vilio na wengine kuzirai akiwepo baba mzazi wa mshitakiwa pia mke wa mshitakiwa aliye kuwa na kichanga hali iliyo pelekea wa huduma wa mahakama kufanya kazi ya kuwa tuliza watu hao.

No comments:

Post a Comment