Tuesday, May 28, 2013
MJAMZITO ALIYEPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA AELEZA KILICHOMPATA BAADA YA KUPOTEA
HAWA NI WANANCHI WA KIJIJI CHA ITUNDUMA WAKIRUDI MAKWAO BAADA YA KUPATIKANA KWA MAMA MJAMZITO ALIYEPOTEA KATIKA HOSPITALI YA KIBENA MJINI NJOMBE ALIYEKUWA AKIJISUBIRIA KUJIFUNGUA.
HUYU NDIYE MAMA MJAMZITO ALIYEKUWA AKITAFUTWA BAADA YA KUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA
AMELALA POLINI KWA MUDA WA SIKU MBILI BILA KUPATA CHAKULA CHOCHOTE NA KULALA KATIKA ENEO LA MSITU WA TANWAT AKIDAI KUONA KWEUSI NA KUTOJITAMBUA
WAUGUZI WA HOSPITALI YA KIBENA AKIWEMO DR EVARISTO MTITU WAKIWA KATIKA CHUMBA AMBACHO MAMA HUYO ALILAZWA BAADA YA KUPATIKANA WAKIWA NA VIONGOZI WA KIJIJI NA MTAA WA KIBENA
word la kujifungulia wanawake katika hospitali ya Kibena
Hatimae Mama Mjamzito Aliekuwa Amepotea Katika Mazingira ya Kutatanisha,Amepatikana Mapema leo Asubuhi Akiwa Katika Misitu ya TANWAT Mjini Njombe.
Mama Huyo Amepatikana Baada ya Msako Mkali Ulioendeshwa na Wananchi wa Kijiji Cha Itunduma Kwa Kushirikiana na Viongozi wa Mitaa ya Kibena.
Wakizungumzia kupatikana kwa mama huyo Viongozi wa Mitaa ya Kibena na Kijiji Cha Itunduma Wamesema Kuwa Mama Huyo Alipatikana Leo Majira ya Saa Tatu Asubuhi Akiwa Kwenye Misitu Hiyo Huku Hali Yake Ikiendelea Vema.
Wamesema Baada ya Kufanikiwa Kumpata Wamemfikisha Hospitali Kwa Uchunguzi Zaidi Wakati Akisubiri Kujifungua
Uongozi huo wa Kijiji cha Itunduma na Kibena wameendelea kuisisitiza serikali kuimarisha ulunzi na usalama katika hospitali hiyo na nkuwataka wananchi kuondoa imani potofu ambazo zilianza kujengeka kwa baadhi ya wananchi juu ya kupotea kwa mama huyo.
Wakizungumza mara baada ya kupatikana kwa mama huyo wananchi wa mitaa ya Kibena na Itunduma wameombe serikali kuimarisha uzio wa kudumu ili kuweka usalama wa wagonjwa na wauguzi katika hospitali hiyo
Aidha wananchi hao wamesema kufatia kutokea kwa tukio hilo liwe changamoto na chachu kwa serikali mkoani Njombe kuona umuhimu wa kuweka uzio kwa haraka kwani asinge patikana mama huyo huenda wananchi wangeweza kuwaelewa vibaya madaktari na manesi wa hospitali hiyo ya Kibena.
Kwa upande wao wauguzi wa hospitali ya Kibena akiwemo dr Evaristo Mtitu wameomba wananchi kuwasiliana na wauguzi kama kuna tatizo limejitokeza hospitalini hapo kabla ya kwenda polisi na kusema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha wa wagonjwa.
Kwa upande wake mama huyo aliyepotea bi Jestina Zabron Mhema alipohojiwa amesema kuwa alipoambiwa na nesi aende kufanya mazoezi alielekea katika barabara ya lami ambapo baada ya kufika hapo alijikuta hali imebadilika haelewi kitu na aliona giza kote hali iliyompelekea kuondoka na kuelekea kwenye msitu ulikuwa jirani na kukaa huko kwa muda wa siku mbili bila kuona chakula akiwa amekaa mpaka leo asubuhi alipopata ufahamu na kuondoka kuelekea hospitali ndipo akakutana na kundi la watu wanamtafuta.
Amesema na yeye amesikitishwa na hali ya sitofahamu iliyomkuta tarehe 26 mwezi huu wa tano .
Mama Huyo Jestina Zabron Mhema Miaka 23 Alipotea May 26 Mwaka Huu Majira ya Saa Sita Mchana Wakati Akiwa Amelazwa Katika Hospitali ya Kibena Mjini Njombe Akisubiri Kujifungua Baada ya Kulazwa Kwa Zaidi ya Wiki Moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment