Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, May 10, 2013

MGOMO WA MADEREVA DALADALA WAWATESA WANANCHI IRINGA LEO, KIONGOZI WA SUMATRA MPYA ABANWA .


Abiria wakigombea  kuingia  daladala  la  wanafunzi leo asubuhi baada ya kuwepo kwa mgomo

Wananchi Iringa mjini wakihangaika kwa usafiri  leo .CHANZO FRANCIS GODWIN IRINGA

MGOMO  wa daladala katika Manispaa ya Iringa umechukua  sura mpya baada ya madereva hao kuamua kueleza uozo uliopo katika ofisi za Sumatra mkoa wa Iringa kuwa wakimkataa ofisa mpya wa Sumatra  mkoa  wa Iringa Rahim Kondo.

Huku  mwenyewe akiwaangukia madereva  hao kwa  kuwaomba radhi baada ya kubanwa na kamati ya usalama barabarani mkoa  kuwaomba radhi madereva  hao.

Madereva hao ambao  leo waligoma  kutoa huduma ya usafiri kwa zaidi ya masaa 9 waliieleza kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa chini ya mwenyekiti wake Salim Asas  kuwa wamechoka kunyanyasika na ofisa  huyo  wa Sumatra mkoa  wa Iringa

Wakizungumza katika  kikao cha pamoja kati ya kamati hiyo ya  usalama barabarani ,madereva na  wamiliki  wa daladala mjini Iringa kikao  kilichofanyika ukumbi wa Olofea mjini hapa kuanzia majira ya 5 asubuhi  hadi saa 9 Alasiri madereva hao  walioma SUMATRA Taifa  kumrejesha ofisa wa Sumatra aliyekuwepo awali Daniel Chilongani na sio huyo wa  sasa.

 

Sababu kubwa ambazo  zilipelekea  daladala  kugoma  ni pamoja na  kuzuiwa kuegesha kwa muda  daladala  eneo la Posta na stendi ya  Miyomboni , pia kutozwa faini kubwa  ukilinganisha na faini halali ya Sumatra pamoja na  kutumia lugha  ya kashfa ikiwa ni pamoja na kuwalinganisha madereva na  wafanyakazi wa ndani  wa  kike.



 Mwenyekiti  wa baraza la usalama barabarani mkoa wa Iringa  Bw.Salim Abri  Asas akimaliza utata kati ya  Sumatra na madereva Iringa
..............................................................................................................................................

Walisema  kuwa hawajapendezwa na utendaji kazi wa Sumatra ikiwa ni pamoja na kumtaka kuondoka mkoa wa Iringa kutokana na kushindwa kuifanya kazi hiyo kwa misingi inayokusudiwa.


Kwani wamedai kuwa vikwazo mbali mbali ambazo wamekuwa wakivipata madereva mjini Iringa vinasababishwa na utendaji mbovu wa Sumatra mkoa wa Iringa pamoja na baadhi ya askari wa usalama barabarani mkoa wa Iringa ambao wamekuwa wakichangia kuwakandamiza zaidi.


Awali mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas aliwataka madereva hao kutuliza jazba na kueleza madai yao katika kamati hiyo ili kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.

Hata  hivyo  Asas alisema  kuwa kuna haja  ya kuwepo kwa ushiriki wa uwakilishi wa madereva katika  kamati hiyo ya usalama barabarani  mkoa  ili nao  waweze kutoa ushauri  wao kwa mambo yanayowahusu.

Wakati  mwakilishi  wa madiwani  wa  Halmashauri Manispaa ya Iringa Jesca Msambatavangu ambae  pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa alisema  kuwa  kilio  cha madereva hao juu ya stendi ya Miyomboni kuwatoza ushuru mkubwa pamoja na ile ya stendi ya Isakalilo kukosa choo ataifikisha katika  vikao  vya madiwani.

Akijibu tuhuma  zilizoelekezwa kwake mbali ya kuwaomba radhi kwa  lugha yeyote mbaya ambayo amepata  kuitoa  wakati  wa kutimiza  wajibu  wake Ofisa  huyo wa Sumatra  mkoa wa Iringa Bw Kondo alisema  kuwa hajapata  kutoza faini kubwa kuliko  ile  iliyoelekezwa na serikali chini ya  wabunge wa  bunge la jamhuri ya muungano  wa Tanzania.

 

Mbali ya  ofisa  huyo kutolea  ufafanuzi huo bado kamati  hiyo iliagiza daladala zote zilizokamatwa na kupelekwa  polisi kwa kushindwa  kulipa faini ya Sumatra  kutolewa  polisi ,huku vituo hivyo  vilivyofutwa kuendelea  kufanya kazi kama awali.

 Mgomo  huo  ulipelekea  shughuli nyingi  za uzalishaji mali  kutofanyika  huku baadhi ya  wananchi  wakichelewa kwenda makazini na  wanafunzi kukwama katika  vituo  huku usafiri  uliokuwa ukitumika ni bajaji ,pikipiki na gari ndogo binafsi kwa nauli kati ya shilingi 1000 hadi 2000

No comments:

Post a Comment