Wednesday, May 1, 2013
SIKUKUU YA WAFANYA KAZI YA FAANA MKOA WA NJOMBE,BAADA YA SHEREHE KUMALIZIKA MJI WA NJOMBE WAPATWA PIGO KUBWA KWA KUONDOKEWA NA MTUMISHI WAKE WA MAJI,MHANDISI ABDALAH HASSAN MGAMBO.
WAFANYAKAZI KUTOKA MAENEO MBALIMBALI WAKIWA NA MABANGO KWENYE SHEREHE ZA MEI MOSI KIMKOA ZIMEFANYIKIA UWANJA WA SABASABA MJINI NJOMBE KITAIFA ZIMEFANYIKIA MKOA WA MBEYA.
MAANDAMANO YA WATUMISHI YAMEANZIA OFISI ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE HADI UWANJA WA SABASABA NA HAPA WANACHEPUKA KUELEKEA UWANJA WA SABASABA
BURUDANI MBALIMBALI ZILIKUWA ZINAENDELEA UWANJANI HAPO
AKIKABIDHI VYETI VYA UFANYAKAZI BORA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE ,MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA
Katika maadhimisho haya mgeni rasmi alikuwa mkuu wa Wilaya ya Njombe bi. Sarah Dumba kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Njombe kaptaini mstaafu Asseri Msangi. picha na Elia Kayombo mdau wa mtandao huu
Rais Jakaya Kikwete Amewahakikishia Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma Kulipwa Mafao Kwa Wakati Pindi Watakapo Staafu Utumishi wa Umma Kutokana na Michango Yao Wanayokatwa Kwenye Mifuko ya Pensheni.
Rais Kikwte Ameyasema Hayo Wakati Akihutubia Kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi Zilizofanyika Kitaifa Mkoni Mbeya na Kuwataka Watumishia Hao Kutokuwa na Hofu Juu ya Malipo Yao Pensheni Kama Inavyodhaniwa na Baadhi ya Watumishi Hao.
Katika Hotuba Yake Rais Kikete Amesema Serikali Imeendelea Kuboresha Mishahara ya Wafanyakazi Pamoja na Kutatua Changamoto Mbalimbali Zinazowakabili Wafanyakazi Kote Nchini.
Aidha Rais Kikwete Amesema Kwa Sasa Serikali Haidaiwi na Shirika Lolote za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Licha ya Kushangazwa na Taarifa ya Shirika la NSSF Kuwa Inaidai Serikali Zaidi ya Shilingi Bilioni 6 Ambalo ni Deni la Nyuma.
Katika Hatua Nyingine Rais Huyo wa Tanzania Amewataka Wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Kuutumia Uwanja wa Mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe Kwa Shughuliza Kiuchumi.
Kwa mkoa wa Njombe sherehe hizo zimeongozwa na mkuu wa mkoa wa Njombe ambapo mkuu wa wilaya ya Njombe bi Sarah Dumba alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Njombe sherehe zilizofanyikia katika viwanja vya sabasaba mjini Njombe.
Wafanyakazi wa kutoka sehemu mbalimbali mkoani hapa walihudhuria na kuiomba serikali kuboresha maslahi ya walimu pamoja na vifaa vya kazi kwa kwa taasisi zisizo za kiserikali na kuboreshewa mishahara hususani kuzingatia masaa ya ziada ambayo wamekuwa wakizidisha kazini.
Sherehe za Mei Mosi Zimefanyika Nchi Kote Hii Leo Ambapo Kitaifa Zimefanyika Katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mjini Mbeya Chini ya Kauli Mbiu Isemayo KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA WA HAKI NA TABAKA LA WAFANYAKAZI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment